The chat will start when you send the first message.
1Kisha Mfalme Sulemani akawaita mbele zake huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Bwana kutoka Sayuni, Mji wa Daudi.
2Wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa Mfalme Sulemani wakati wa sikukuu ya mwezi wa Ethanimu, ndio mwezi wa saba.
3Wazee wote wa Israeli walipofika, makuhani wakajitwika lile Sanduku,
4nao wakalipandisha Sanduku la Bwana , na Hema la Kukutania, pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani na Walawi wakavibeba,
5naye Mfalme Sulemani na kusanyiko lote la Israeli waliokuwa wamemzunguka wakasimama mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu za kondoo na ngʼombe nyingi kiasi kwamba idadi yao haikuweza kuandikwa au kuhesabika.
6Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la Bwana hadi mahali pake ndani ya mahali patakatifu sana humo Hekaluni, ndipo Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi.
7Makerubi yalitandaza mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kutia kivuli Sanduku pamoja na mipiko yake ya kubebea.
8Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilionekana kutoka Mahali Patakatifu mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo.
9Ndani ya Sanduku hapakuwa na kitu kingine isipokuwa vile vibao viwili vya mawe ambavyo Musa aliviweka ndani yake huko Horebu, mahali Bwana alipofanya agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.
10Makuhani walipoondoka katika Mahali Patakatifu, wingu likajaza Hekalu la Bwana .
11Nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Bwana ulijaza Hekalu lake.
12Ndipo Sulemani akasema, “Bwana alisema kwamba ataishi katika giza nene;
13naam, hakika nimekujengea Hekalu zuri sana, mahali pako pa kuishi milele.”
14Kusanyiko lote la Israeli walipokuwa wamesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki.
15Kisha akasema:
22Kisha Sulemani akasimama mbele ya madhabahu ya Bwana machoni pa kusanyiko lote la Israeli, akanyoosha mikono yake kuelekea mbinguni,
23na kusema:
54Sulemani alipomaliza dua na maombi haya yote kwa Bwana , akainuka kutoka mbele ya madhabahu ya Bwana , mahali alipokuwa amepiga magoti akiwa amenyoosha mikono yake kuelekea mbinguni.
55Akasimama na kubariki kusanyiko lote la Israeli kwa sauti kubwa, akisema:
62Kisha mfalme na Waisraeli wote pamoja naye wakatoa dhabihu mbele za Bwana .
63Sulemani akatoa dhabihu sadaka za amani kwa Bwana : ngʼombe elfu ishirini na mbili, pamoja na kondoo na mbuzi elfu mia moja na ishirini. Ndivyo mfalme na Waisraeli wote walivyoweka wakfu Hekalu la Bwana .
64Siku hiyo hiyo mfalme akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la Bwana , na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na mafuta ya wanyama wa sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za Bwana ilikuwa ndogo sana kuweza kubeba sadaka hizo za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na mafuta ya wanyama wa sadaka za amani.
65Hivyo Sulemani akaiadhimisha sikukuu kwa wakati ule, na Waisraeli wote pamoja naye: walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri. Wakaiadhimisha mbele za Bwana Mungu wetu kwa siku saba na siku saba zaidi, yaani jumla siku kumi na nne.
66Siku iliyofuata, aliwaruhusu watu waondoke. Wakambariki mfalme, kisha wakaenda nyumbani wakiwa na mashangilio na furaha moyoni kwa ajili ya mambo yote mema ambayo Bwana alimtendea kwa ajili ya Daudi mtumishi wake na watu wake Israeli.