3 Yohana 1

3 Yohana 1

Salamu

Gayo anatiwa moyo

2Mpendwa, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo.

3Ilinifurahisha sana baadhi ya ndugu walipokuja na kutueleza kuhusu uaminifu wako katika kweli na jinsi unavyoendelea kuenenda katika hiyo kweli.

4Sina furaha kubwa kuliko hii, ya kusikia kwamba watoto wangu wanaenenda katika kweli.

5Rafiki mpendwa, wewe ni mwaminifu kwa yale unayowatendea ndugu, ingawa wao ni wageni kwako.

6Wameshuhudia kuhusu upendo wako mbele ya kanisa. Utafanya vyema ukiwasafirisha kama inavyostahili kwa Mungu.

7Ilikuwa ni kwa ajili ya hilo Jina waliondoka, bila kukubali kupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasiomwamini Kristo.

8Kwa hiyo imetupasa sisi kuonesha ukarimu kwa watu kama hao ili tuweze kutenda kazi pamoja kwa ajili ya kweli.

Deotrefe anakemewa

9Nililiandikia kanisa, lakini Deotrefe, yeye apendaye kujifanya wa kwanza, hakubali mamlaka yetu.

10Hivyo nikija, nitakumbuka matendo yake atendayo, akitusingizia kwa maneno ya hila. Wala hatosheki na hayo anayotusingizia, bali pia hukataa kuwakaribisha ndugu, na hata huwazuia wale walio tayari kufanya hivyo na kuwafukuza watoke kanisani.

Demetrio anasifiwa

11Rafiki mpendwa, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Yeyote atendaye mema anatoka kwa Mungu, bali atendaye mabaya hajamwona Mungu.

12Kila mtu ameshuhudia mema kuhusu Demetrio, vivyo hivyo hata na hiyo kweli yenyewe. Sisi pia twashuhudia mema juu yake, nanyi mwajua kwamba ushuhuda wetu ni kweli.

Hitimisho

13Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kuandika kwa kalamu na wino.

14Badala yake, nataraji kukuona upesi, nasi tutaongea pamoja ana kwa ana.

15Amani iwe kwako.

Rafiki zetu walio hapa wanakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu walio huko, kila mmoja kwa jina lake.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.