The chat will start when you send the first message.
5Lakini jeshi la Wakaldayo wakawafuatia na kumpata Sedekia katika nchi tambarare za Yeriko. Wakamkamata na kumpeleka kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, ambapo alimtangazia hukumu.
6Huko Ribla, mfalme wa Babeli aliwachinja wana wa Sedekia mbele ya macho yake, na pia akawaua wakuu wote wa Yuda.
7Kisha akayangʼoa macho ya Sedekia na kumfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli.
8Jeshi la Wakaldayo likachoma moto jumba la kifalme na nyumba za watu, na kuzibomoa kuta za Yerusalemu.
9Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme akawachukua na kuwapeleka uhamishoni Babeli watu waliokuwa wamebaki ndani ya mji, pamoja na wale waliokuwa wamejisalimisha kwake, na watu wengine wote.
10Lakini Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi aliwabakiza baadhi ya watu maskini katika nchi ya Yuda, ambao hawakuwa na kitu. Naye wakati huo akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba mengine.
11Basi, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa ametoa maagizo kuhusu Yeremia kupitia Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme akisema:
12“Mchukue umtunze. Usimdhuru, lakini umfanyie chochote anachotaka.”
13Basi Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi, Nebushazbani afisa mkuu, Nergal-Shareza afisa wa cheo cha juu, na maafisa wengine wote wa mfalme wa Babeli
14wakatuma watu kumwondoa Yeremia kutoka ua wa walinzi. Wakamkabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, ili amrudishe nyumbani mwake. Kwa hiyo akabaki miongoni mwa watu wake mwenyewe.
15Yeremia alipokuwa amezuiliwa katika ua wa walinzi, neno la Bwana lilimjia kusema:
16“Nenda ukamwambie Ebed-Meleki Mkushi, ‘Hili ndilo Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kutimiza maneno yangu dhidi ya mji huu kwa maafa, wala si kwa mema. Wakati huo, hayo yatatimizwa mbele ya macho yako.
17Lakini siku hiyo nitakuokoa, asema Bwana ; hutatiwa mikononi mwa wale unaowaogopa.
18Nitakuokoa; hutaanguka kwa upanga, maisha yako yatakuwa salama, kwa sababu unanitumaini, asema Bwana .’ ”