Hesabu 3

Hesabu 3

Walawi

1Hivi ndivyo vizazi vya Haruni na Musa kwa wakati ambao Bwana alizungumza na Musa katika Mlima Sinai.

2Majina ya wana wa Haruni yalikuwa: Nadabu mzaliwa wa kwanza na Abihu, Eleazari na Ithamari.

3Hayo yalikuwa majina ya wana wa Haruni, makuhani wapakwa mafuta, waliokuwa wamesimikwa kuhudumu kama makuhani.

4Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele za Bwana walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari walihudumu peke yao kama makuhani wakati wote wa maisha ya Haruni baba yao.

5Bwana akamwambia Musa,

6“Walete kabila la Lawi mbele ya Haruni kuhani ili wamsaidie.

7Watafanya huduma kwa ajili yake na kwa jumuiya yote katika Hema la Kukutania kwa kufanya kazi za Maskani.

8Watatunza samani zote za Hema la Kukutania, wakitimiza wajibu wa kuhudumia Waisraeli kwa kufanya kazi ya Maskani.

9Wakabidhi Walawi kwa Haruni na wanawe; hao ndio Waisraeli ambao wanakabidhiwa kwake kabisa.

10Waweke Haruni na wanawe kuhudumu kama makuhani; mtu mwingine yeyote atakayesogea mahali patakatifu atauawa.”

11Bwana akamwambia Musa,

12“Nimewatwaa Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli badala ya mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila mwanamke wa Mwisraeli. Walawi ni wangu,

13kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza ni wangu. Nilipowaua wazaliwa wa kwanza huko Misri, nilimtenga kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli awe wangu, akiwa mwanadamu au mnyama. Watakuwa wangu. Mimi ndimi Bwana .”

14Bwana akamwambia Musa katika Jangwa la Sinai,

15“Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.”

16Kwa hiyo Musa akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno la Bwana .

17Haya yalikuwa majina ya wana wa Lawi:

18Haya ndio yaliyokuwa majina ya koo za Wagershoni:

19Koo za Wakohathi zilikuwa ni:

20Koo za Wamerari zilikuwa ni:

22Idadi ya wanaume wote wa umri wa mwezi mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa elfu saba na mia tano.

23Ukoo wa Wagershoni walitakiwa kuweka kambi zao upande wa magharibi, nyuma ya Maskani.

24Kiongozi wa jamaa za Wagershoni alikuwa Eliasafu mwana wa Laeli.

25Katika Hema la Kukutania, Wagershoni walikuwa na wajibu wa kutunza Maskani na hema, vifuniko vyake, pazia katika mlango wa kuingilia ndani ya Hema la Kukutania,

26mapazia ya ua, pazia katika ingilio la ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pamoja na kamba, na kila kinachohusika kwa matumizi yake.

28Hesabu ya wanaume wote wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walikuwa elfu nane na mia sita.

Wakohathi waliwajibika kutunza mahali patakatifu.

29Koo za Wakohathi zilitakiwa kuweka kambi zao upande wa kusini wa Maskani.

30Kiongozi wa jamaa za koo za Wakohathi alikuwa Elisafani mwana wa Uzieli.

31Waliwajibika kutunza Sanduku la Agano, meza, kinara cha taa, madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu vinavyotumika kuhudumu, pazia, na kila kitu kinachohusika na matumizi yake.

32Kiongozi mkuu wa Walawi alikuwa Eleazari mwana wa kuhani, Haruni. Aliwekwa juu ya wale waliowajibika kutunza mahali patakatifu.

34Hesabu ya wanaume wote wenye umri wa mwaka mmoja au zaidi waliohesabiwa, walikuwa elfu sita na mia mbili.

35Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili.

Hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani.

36Wamerari waliwekwa kutunza miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo, vitako na vifaa vyake vyote na kila kitu kilichohusika na matumizi yake,

37na pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake.

38Musa, na Haruni na wanawe walitakiwa kuweka kambi zao mashariki mwa Maskani, kuelekea mawio ya jua, mbele ya Hema la Kukutania.

Wao walihusika na utunzaji wa mahali patakatifu kwa niaba ya Waisraeli.

Mtu mwingine yeyote aliyepasogelea mahali patakatifu angeuawa.

40Bwana akamwambia Musa, “Wahesabu wazaliwa wa kwanza wa kiume wote wa Waisraeli wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi na uorodheshe majina yao.

41Nitwalie Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya wazaliwa wa mifugo ya Waisraeli. Mimi ndimi Bwana .”

42Hivyo Musa akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa Waisraeli, kama Bwana alivyomwamuru.

43Jumla ya hesabu ya wazaliwa wa kwanza wanaume wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walioorodheshwa kwa majina, walikuwa elfu ishirini na mbili na mia mbili na sabini na watatu (22,273).

44Bwana akamwambia Musa,

45“Watwae Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya mifugo yao. Walawi watakuwa wangu. Mimi ndimi Bwana .

46Ili kukomboa wazaliwa wa kwanza mia mbili na sabini na watatu (273) wa Waisraeli ambao wamezidi hesabu ya Walawi,

47kusanya shekeli tano kwa kila mmoja, kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.[#3:47 Shekeli tano ni sawa na gramu 55.; #3:47 Gera 20 ni sawa na gramu 11.]

48Mpe Haruni na wanawe hizo fedha kwa ajili ya ukombozi wa idadi ya Waisraeli waliozidi.”

49Kwa hiyo Musa akakusanya fedha za ukombozi kutoka kwa wale ambao hesabu yao ilizidi wale waliokombolewa na Walawi.

50Kutokana na wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli alikusanya fedha yenye uzito wa shekeli elfu moja na mia tatu sitini na tano (1,365) kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu.[#3:50 Shekeli 1,365 ni sawa na kilo 15.5.]

51Musa akampa Haruni na wanawe ile fedha ya ukombozi, kama alivyoamriwa na neno la Bwana .

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.