Hesabu 33

Hesabu 33

Vituo katika safari ya Waisraeli

1Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Musa na Haruni.

2Kwa agizo la Bwana , Musa aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:

50Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani, ngʼambo ya Yeriko, Bwana akamwambia Musa,

51“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani,

52wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kusubu, na kubomoa mahali pao pa juu pa kuabudia.

53Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki.

54Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.

55“ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wa nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi.

56Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.