The chat will start when you send the first message.
1Wamenitesa sana tangu ujana wangu;
Israeli na aseme sasa:
2wamenitesa sana tangu ujana wangu,
lakini bado hawajanishinda.
3Wakulima wamelima mgongo wangu,
na kufanya mifereji yao mirefu.
4Lakini Mwenyezi Mungu ni mwenye haki;
amenifungua toka kamba za waovu.
5Wale wote wanaoichukia Sayuni
na warudishwe nyuma kwa aibu.
6Wawe kama majani juu ya paa,
ambayo hunyauka kabla hayajakua;
7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,
wala akusanyaye kujaza mikono yake.
8Wale wapitao karibu na wasiseme,
“Baraka ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako;
tunakubariki katika jina la Mwenyezi Mungu.”