The chat will start when you send the first message.
1Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Mwenyezi Mungu.
2Ee Bwana, sikia sauti yangu.
Masikio yako na yawe masikivu
kwa kilio changu unihurumie.
3Kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ungeweka kumbukumbu ya dhambi,
Ee Bwana, ni nani angeweza kusimama?
4Lakini kwako kuna msamaha,
kwa hiyo wewe unaogopwa.
5Namngojea Mwenyezi Mungu, nafsi yangu inangojea,
katika neno lake naweka tumaini langu.
6Nafsi yangu inamngojea Bwana
kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,
naam, kuliko walinzi
waingojeavyo asubuhi.
7Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungu,
maana kwa Mwenyezi Mungu kuna upendo usiokoma,
na kwake kuna ukombozi kamili.
8Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli
kutoka dhambi zao zote.