Zaburi 11

Zaburi 11

Wimbo wa kumtumainia Mungu

1BWANA ndiye niliyemkimbilia.

Mbona mnaiambia nafsi yangu,

Kimbia kama ndege mlimani kwenu?

2Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta,

Wanaitia mishale yao katika uta,

Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.

3Kama misingi ikiharibika,

Mwenye haki atafanya nini?

4BWANA yu katika hekalu lake takatifu.[#Hab 2:20; Efe 5:13; Ebr 4:13]

BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni,

Macho yake yanaangalia;

Kope zake zinawapima wanadamu.

5BWANA humjaribu mwenye haki;[#Ayu 5:17; Zab 94:12]

Bali nafsi yake humchukia asiye haki,

Na mwenye kupenda udhalimu.

6Awanyeshee wasio haki mitego,

Moto na kiberiti na upepo wa joto

Na viwe fungu la kikombe chao.

7Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki,

Apenda matendo ya haki,

Wanyofu wa moyo watauona uso wake.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 
Published by: Bible Society of Tanzania