Zaburi 117

Zaburi 117

Mwito wa wote kuabudu

1Haleluya.[#Rum 15:11]

Enyi mataifa yote, msifuni BWANA,

Enyi watu wote, mhimidini.

2Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu,

Na uaminifu wa BWANA ni wa milele.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 
Published by: Bible Society of Tanzania