The chat will start when you send the first message.
1Watu wote wa eneo lote la magharibi wakampelekea mfalme Nebukadneza ujumbe wa amani, wakisema,
2“Sisi tunabaki kuwa watiifu kwako mfalme mkuu Nebukadneza. Tumo mikononi mwako na tu tayari kukutii na kukutumikia jinsi upendavyo.
3Majengo yetu, nchi yetu yote, mashamba yetu ya ngano, mifugo wetu na mahema yetu vipo chini ya mamlaka yako; vitumie upendavyo.
4Watu wetu ni watumwa wako, na unaweza kuitumia miji yetu upendavyo.”
5Baada ya wajumbe wa amani kuleta ujumbe wenyewe,
6Holoferne aliliongoza jeshi hadi pwani ya bahari ya Mediteranea. Akaweka ulinzi kwenye miji yote iliyozungushiwa kuta na kuchagua wanaume wenyeji kuwa jeshi la akiba.
7Watu wote pamoja na wale wa nchi jirani walimkaribisha Holoferne kwa ngoma huku wamevaa taji za maua.
8Lakini Holoferne alipabomolea mbali mahali pao pote pa ibada na kukatilia mbali miti yao mitakatifu. Alifanya hivyo kwa sababu alikuwa ameagizwa kuvunjilia mbali sanamu zote za miungu ili mataifa yamwabudu Nebukadneza peke yake, na kwamba watu wa kila lugha na taifa wamwite mungu wao.[#Taz Kut 34:13; 2 Nya 17:6]
9Kisha, Holoferne akapita katikati ya Bonde la Yezreeli karibu na Dothani, mkabala na milima ya Yuda.
10Akapiga kambi kati ya miji ya Geba na Sithopoli. Akakaa huko ili kukusanya vifaa vya jeshi lake.