Amosi 2

Amosi 2

Yatakayowapata Wamoabu, Wayuda na Waisiraeli.

1Hivi ndivyo, Bwana anavyosema:

Kwa ajili ya mapotovu ya Moabu matatu au manne

sitayarudisha, yasiwapate,

kwa kuwa mifupa ya mfalme wa Edomu waliichoma moto,

hata ikawa chokaa.

2Nitatupa moto kwao Moabu, uyale majumba ya Kerioti,

nao Wamoabu watakufa katika mvurugo,

makelele ya vita na milio ya mabaragumu ikisikilika.

3Naye mwamuzi nitamng'oa katikati yao,

nao wakuu wao wote nitawaua pamoja nao.

Bwana ameyasema.

4Hivi ndivyo, Bwana anavyosema:

Kwa ajili ya mapotovu ya Yuda matatu au manne

sitayarudisha, yasiwapate,

kwa kuwa wameyakataa Maonyo ya Bwana,

wakaacha kuyashika maongozi yake,

ikawapoteza miungu yao ya uwongo baba zao waliyoifuata.

5Nitatupa moto kwao Yuda, uyale majumba ya Yerusalemu.

6Hivi ndivyo, Bwana anavyosema:

Kwa ajili ya mapotovu ya Isiraeli matatu au manne

sitayarudisha, yasiwapate,

kwa kuwa wamewauza waongofu kwa fedha,

nao maskini kwa viatu viwili.

7Wanatunukia na kutwetatweta,

mavumbi ya nchi yawe vichwani juu yao wakiwa,

nazo njia za wanyonge huzipotoa.

Mtu na baba yake pamoja humwendea mwanamke mgoni,

Jina langu takatifu walipatie uchafu.

8Hutumia nguo, walizopewa za kuwekea wengine,

hujitandikia zizo hizo pote, wanapotambikia;

nyumbani mwa miungu yao hunywa mvinyo zao,

walizotozwa kuwa malipo ya makosa.

9Nami ndimi niliyewaangamiza Waamori mbele yao,

ndio waliokuwa warefu kama miangati mirefu na wanguvu

kama mivule,

nikayaangamiza mazao yao ya juu nayo mizizi yao ya chini.

10Nami ndimi niliyewatoa katika nchi ya Misri na kuwaleta

huku,

nikawaongoza miaka arobaini nyikani,

nikawapa nchi ya Waamori, iwe nchi yenu.

11Namo miongoni mwa wana wenu nikainua wengine, wawe

wafumbuaji,

nao wengine nikawachagua katika vijana wenu, wajieue kuwa

wangu.

Au sivyo vilivyokuwa, ninyi wana wa Isiraeli?

ndivyo, asemavyo Bwana.

12Nao waliojieua mliwanywesha mvinyo,

nao wafumbuaji mkawaagiza kwamba: Msifumbue!

13Mtaniona, nikiwalemea, kama gari linavyolemewa likijaa

miganda.

14Ndipo, mwenye miguu izoeayo mbio atakaposhindwa na

kukimbia,

naye mwenye nguvu hataweza kutumia hizo nguvu zake kuu,

wala fundi wa vita hataiponya roho yake,

15wala mshika upindi hatasimama,

wala mwenye miguu miepesi hatapona,

wala mpanda farasi hataiponya roho yake.

16Naye aushupazaye moyo wake kwa mafundi wa vita

siku hiyo atakimbia akiwa uchi;

ndivyo, asemavyo Bwana.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania