The chat will start when you send the first message.
1Kale Mungu alisema na baba zetu vinywani mwa wafumbuaji mara nyingi na kufuata njia.
2Siku hizi za mwisho amesema na sisi kinywani mwa Mwanawe, aliyemweka kuwa kibwana chao yaliyo yake yote. Yeye ndiye, ambaye aliumba naye hata ulimwengu wote.[#Sh. 2:8; Yoh. 1:3; Kol. 1:16.]
3Huyu hutuangazia utukufu wake, kwani kama Mungu alivyo, ndivyo, naye alivyo; tena yeye huvitunza vyote kwa Neno lake lenye nguvu. Alipokwisha kutupatia osho liyaondoalo makosa, akaketi kuumeni kwa mwenye ukuu mbinguni juu,[#Ebr. 9:14,26; Mat. 26:64; Mar. 16:19; 2 Kor. 4:4; Kol. 1:15-16.]
4akapata kuwa mtukufu kuliko malaika kwa hivyo, alivyorithi Jina linalolipita lao.[#Fil. 2:9.]
5Kwani yuko malaika, Mungu aliyemwambia siku iwayo yote:
Wewe ndiwe Mwanangu,
siku hii ya leo mimi nimekuzaa?
Na tena:
Mimi nitakuwa baba yake,
naye atakuwa mwanangu?
6Kwa ajili ya siku, alipotaka kumwingiza mzaliwa wake wa kwanza tena ulimwenguni, anasema:
Malaika wote wa Mungu sharti wamwangukie yeye!*
7Mambo ya malaika anayasema kwamba:
Huwatumia malaika zake kuwa upepo
nao watumishi wake kuwa mioto iwakayo.
8Lakini mambo ya mwana anayasema kwamba:
Mungu, kiti chako cha kifalme kiko kale na kale pasipo mwisho,
nayo fimbo ya ufalme wako ndiyo fimbo inyoshayo mambo ya watu.
9Wewe ulipenda wongofu, ukachukia upotovu.
Kwa hiyo Mungu aliye Mungu wako
alikupaka mafuta ya kufurahisha kuliko yale ya wenzio.
10Tena anasema:
Wewe Bwana, mwanzoni uliiweka misingi ya nchi,
mbingu nazo ni kazi ya mikono yako wewe.
11Hizo zitaangamia, lakini wewe unafuliza kuwapo.
Kweli, zote zitachakaa kama nguo,
12nawe utazizinga kama nguo ya kujitandia;
zitachujuka kama nguo.
Lakini wewe ndiwe yuleyule uliyekuwa,
miaka yako haitakoma.
13Lakini yuko malaika, aliyemwambia po pote:
keti kuumeni kwangu,
mpaka niwaweke adui zako
chini miguuni pako?
14Hawa wote si roho tu za kutumika zitakazotumwa kuwatumikia wale watakaourithi wokovu?[#Sh. 34:8; 91:11; Dan. 7:10.]