The chat will start when you send the first message.
1Sasa tusemeane nanyi wenye mali: Lieni na kuyaombolezea mahangaiko yenu yatakayowapata![#Luk. 6:24; 12:15.]
2Mali zenu zimeoza, nguo zenu zimeliwa na mende.[#Mat. 6:19.]
3Dhahabu zenu na fedha zenu zimeingiwa na kutu, nazo kutu zao zitawasuta, zitawala nyama za miili yenu kama moto. Mmelimbika mali nyingi siku hizi za mwisho.
4Angalieni, malipo, mliyowanyima wakulima wa mashambani kwenu, yanalia, nayo malalamiko ya wavunaji yamefika masikioni mwa Bwana Mwenye vikosi.[#5 Mose 24:14-15.]
5Mmeyala mazuri yaliyoko nchini na kutapanya mali. Mioyo yenu mmeinonesha siku za kuchinja nyama.[#Yer. 12:3; 25:34; Luk. 16:19,25.]
6Mwongofu mmemhukumu, mkamwua; naye hakuwabishia.[#Yak. 2:6.]
7Ndugu, vumilieni, mpaka Bwana atakaporudi! Tazameni, mkulima anavyoyangoja mazao ya nchi, maana ni yenye kima! Huvumilia mpaka apate mvua ya vuli nayo ya masika.[#Luk. 21:19; Ebr. 10:36.]
8Vumilieni nanyi, mwitie mioyo yenu nguvu! Kwani kurudi kwake Bwana kumekaribia.
9Ndugu, msinung'unikiane ninyi kwa ninyi, msipate kuhukumiwa! Tazameni, mhukumu amesimama milangoni mwenu!
10Ndugu, wafumbuaji waliosema kwa nguvu ya Jina la Bwana washikeni kuwa vielezo vya kujifunzia kuteseka vibaya na kuvumilia![#Mat. 5:12.]
11Tazameni, twawatazamia wavumiliao kuwa wenye shangwe! Mmesikia, Iyobu alivyovumilia, nao mwisho wa Bwana mmeuona, kwani Bwana huonea wengi uchungu na upole.[#Iy. 1:21-22; 42:1-16.]
12Ndugu zangu, nilitakalo sana, ni hili la kwamba: Msiape! Msiape na kutaja wala mbingu wala nchi wala kiapo kingine cho chote! Mkisema: Ndio, iwe ndio kweli. Tena mkisema: Sio, iwe sio kweli, kwamba msitumbukie hukumuni![#Mat. 5:34-37.]
13*Kwenu kama yuko mwenye kuteseka, na amwombe Mungu! Kama yuko mwenye kutulia, na aimbe nyimbo![#Sh. 50:15; Kol. 3:16.]
14Kama yuko mwenye kuugua, na awaite wazee wa wateule, wamwombee, tena wampake mafuta katika Jina la Bwana![#Mar. 6:13;; Luk. 10:34.]
15Wakimwombea kwa kumtegemea Mungu, vitamwokoa yule mgonjwa, naye Bwana atamwinua tena; kama yuko na makosa, aliyoyafanya, ataondolewa.[#Mar. 16:18.]
16Jiungamianeni makosa ninyi kwa ninyi na kuombeana, mpate kupona! Kuomba kwake mwongofu kuko na nguvu nyingi kukiwa kwa kweli.
17Elia alikuwa mtu aliyeteseka kama sisi; naye alipomwomba Mungu, mvua isinye, ndipo, mvua ilipoacha kunya nchini miaka mitatu na miezi sita.[#1 Fal. 17:1; Luk. 4:25.]
18Alipoomba tena, ndipo, mbingu ziliponyesha mvua, nayo nchi ikayachipuza mazao yake.[#1 Fal. 18:42.]
19Ndugu zangu, kama kwenu yuko aliyepotea na kuyaacha yaliyo ya kweli, tena mwingine akimrudisha,[#Gal. 6:1.]
20tambueni: mwenye kurudisha mkosaji, aiache ilenjia yake ya upotevu, huiokoa roho yake kufani na kufunika makosa mengi!*[#Sh. 51:15; Fano. 10:12; 1 Petr. 4:8.]