The chat will start when you send the first message.
1Maneno mengi kama hayo yasijibiwe?
2Au mtu ajuaye kusema hivyo atakuwa mwongofu?
3Watu wengine wayanyamazie tu mapuzi yako, asioneke mtu atakayekutweza, wewe ukimfyoza?
4Wewe tu useme: Maelezo yangu ni ya kweli, nami nimetakata machoni pako?[#Iy. 9:21; 10:7.]
5Laiti Mungu akutolee maneno kwa kusema na kuifumbua midomo yake, akushinde![#Iy. 38:1.]
6Akakufunulia navyo vilindi vya ujuzi wa kweli vilivyofichwa, kwani mizungu iliyomo hufaa mara mbili; ndipo, utakapojua, ya kuwa Mungu amekuondolea manza, ulizozikora.[#Sh. 51:8.]
7Je? Waweza kuuvumbua mwanzo wake Mungu usiochunguzika? Au waweza kuyapambazua yake Mwenyezi yatakayokuwa ya mwisho?
8Yakiwa juu mbinguni, utafanyaje? Yakiwa chini ndani kupita kuzimuni, utajuaje?
9Ukitaka kuupima urefu wake, unaupita wa nchi, nao upana wake unaupita wa bahari.
10Yeye akitokea na kupita, afunge watu, yuko nani awezaye kumrudisha nyuma, aliyempeleka shaurini?
11Kwani yeye anawajua wasiofaa kitu, huwaona waovu, ijapo asiwaangalie.
12Hapo naye mwenye kichwa kikosacho akili sharti aerevuke, kwani mtu huwa kama mwana wa punda wa nyikani siku akizaliwa.
13Kama wewe ungeulinganya vema moyo wako, na kumkunjulia mikono yako,
14kama ungeuondoa uovu uliomo mkononi mwako, ujiendee mbali, kama ungeukataza upotovu kukaa hemani mwako,
15basi, ungeweza kuuinua uso wako pasipo uchafu wo wote; kwa kuwa umeshikizwa vema, usiogope cho chote!
16Ndipo, wewe utakapoyasahau nayo masumbuko, yatakuwa kama maji yaliyokupwa hapo, utakapoyakumbuka.
17Ndipo, utakapotokewa na siku ziangazazo kuliko jua la mchana, napo palipokuwa na giza patakuwa kama mapambazuko.
18Kwa kuwa na kingojeo utapata cha kukijetea, utakapochungulia nyumbani mwako utalala na kutulia.
19Tena hatakuwako atakayekustusha hapo, utakapolala, nao wengi watajipendekeza usoni kwako.[#Sh. 3:6; 4:8.]
20Lakini macho yao wasiomcha Mungu yataingiwa na kiwi, mahali pa kupakimbilia patawapotelea, kingojeo chao kitakuwa hiki tu: kutoa roho.[#Iy. 8:13.]
Iyobu akajibu akisema: