The chat will start when you send the first message.
1Nilifanya agano na macho yangu, kisha ningewezaje kumtazama mwanamwali kwa kumtamani?[#Mat. 5:28-29.]
2Kwani Mungu huko juu angalinipatia nini? Yeye Mwenyezi angalitoa fungu gani mbinguni, liwe langu?
3Je? Wapotovu fungu lao sio mwangamizo? Nao wafanyao maovu fungu lao sio machukivu?
4Yeye hazioni hizo njia zangu? Wala hazihesabu nyayo zangu?[#Iy. 23:10.]
5Kama nilifanya mwenendo ulio wa uwongo, miguu yangu ikakimbilia yaliyo madanganyifu,
6Mungu na anipime kwa mizani iliyo sawa; ndipo, atakapojua, ya kuwa sikukosa.
7Kama nyayo zangu ziliiacha njia yake, kama moyo wangu ulizifuata tamaa za macho yangu, kama uchafu wo wote uligandamana na mikono yangu:[#Sh. 7:4-6.]
8basi, mimi nitakayoyapanda, mwingine na ayale, nayo mazao yangu na yang'olewe pamoja na mizizi yao!
9Kama moyo wangu uliingiwa na tamaa ya mke wa mwingine, mpaka nikaja kumwotea mlangoni pake mwenzangu,
10mke wangu na amsagie mwingine unga wake, hata wengine na waje kulala naye.[#5 Mose 28:30; 2 Sam. 12:11.]
11Kwani hili lingekuwa kosa lililo baya zaidi, ni kukora manza zipasazo kuhukumiwa na waamuzi wakuu.
12Hivyo ningalijipatia moto wa kunila hata kuzimuni, nao ungaliyaangamiza yote pia, niliyoyapata.
13Kama nilikataa shauri la mtumishi wangu wa kiume au wa kike, walipotaka kushindana na mimi mwenyewe,
14ningefanya nini, Mungu akininukia? au ningemjibu nini, akiyakagua?
15Je? Aliyenitengeneza tumboni mwa mama hakumtengeneza naye? Siye yeye mmoja aliyetuumba kuwa mimba?[#Ef. 6:9.]
16Wanyonge niliwanyima walichokitaka kwangu? Au nilizimisha macho yaliyokuwa ya mjane?[#Iy. 29:12.]
17Au nililila tonge langu peke yangu, afiwaye na wazazi asile naye?
18Sivyo, ila tangu ujana wangu alikulia kwangu kama kwa baba yake, toka hapo nilipotoka tumboni mwa mama yangu niliwaongoza wajane.
19Hapo nilipoona mtu, akifa kwa kukosa nguo, au maskini akikosa lo lote la kujifunika,[#Yes. 58:7.]
20basi, viuno vyake havikunibariki, alipojipatia kijoto kwa nguo za nywele za kondoo wangu?
21Kama nilikemea mwana aliyefiwa na wazazi nikimkunjulia mkono kwa kuona wanaonisaidia langoni penye mashauri,[#Iy. 29:7.]
22bega langu na lianguke kwa kuteuka mahali pake, nalo fupa la mkono wangu na livunjike kiungoni mwake!
23Kwani mwangamizo wa Mungu ungalinistusha, nisiweze kusema neno kwa hivyo, anavyotukuka.[#Iy. 32:22.]
24Kama nilitumia dhahabu kuwa egemeo langu, na kuziwazia zile dhahabu safi kuwa kimbilio langu,[#Sh. 52:9.]
25kama niliufurahia wingi wa mali zangu, kwa kuwa mkono wangu ulipata vingi vya kuvilimbika,
26kama hapo, nilipolitazama jua, jinsi linavyoangaza, au mwezi, jinsi unavyoendelea ukiwa na utukufu wake,[#5 Mose 4:19.]
27kama hapo moyo wangu huko ndani ulitamani kutambika, mpaka kinywa changu kikakinonea kiganja changu:[#1 Fal. 19:18.]
28huko ningekora manza zipasazo kuhukumiwa na waamuzi wakuu, kwani huko ningemkana Mungu wa huko juu kuwa Mungu wangu.
29Je? Nilimfurahia mchukivu wangu, alipoteswa? Au nilishangilia, mabaya yalipompata?[#Sh. 35:12; Fano. 24:17.]
30Sikukipa kinywa changu ruhusa kukosa hivyo, kije kuiapiza roho yake, ishuke kuzimuni.[#1 Petr. 3:9.]
31Walioingia hemani mwangu hawasemi: Yuko mtu asiyeshibishwa na nyama, alizompa?
32Kweli kwangu hakuwako mgeni aliyelala nje, mimi humfungulia mpitaji milango yangu.[#1 Mose 19:2; Ebr. 13:2.]
33Je? Niliyafunika mapotovu yangu kama watu wengine? Au nilizificha manza, nilizozikora, kifuani pangu?
34Je? Pako, nilipoogopa wingi wa watu? Au yalinistusha mazomeo ya milango yao, hata nikanyamaza, nisitoke nyumbani?
35Kama ningepata mtu atakayenisikiliza, ningemwonyesha maandiko yangu, Mwenyezi anijibu. Kiko nacho kitabu, alichokiandika mwenye kunigombeza;[#Iy. 23:3-7.]
36kweli hicho ningekichukua begani pangu, au ningekifunga kichwani pangu kuwa kilemba changu.
37Ningemsimulia hesabu ya nyayo zangu, tena ningekuwa kama mkuu wa watu, nimkaribie.
38Kama shamba langu linanisuta na kupiga kelele, kama matuta yake yanaitikia na kulia,
39kama niliyala mazao yake pasipo kulipa na kuizimisha roho yake mwenye shamba,[#Iy. 24:11.]
40basi, penye ngano na patokee mangugi matupu, napo penye mawele ndago tu! Maneno, Iyobu aliyoyasema, yamekwisha.