The chat will start when you send the first message.
1Kama yangepimwa machafuko yangu,
2wakiyatia nayo mateso yangu katika mizani,
3haya yangetokea kuwa mazito zaidi kuliko mchanga wa baharini; kwa hiyo maneno yangu ni ya kupotelewa tu.
4Kwani mishale ya Mwenyezi imenipiga, nayo sumu yao yenye moto roho yangu ikainywa, vitisho vya Mungu vikajipanga kuninasa mimi.[#Sh. 38:3.]
5Je? Punda wa porini hulia mbugani penye majani? Au yuko ng'ombe apigaye kelele penye chakula chake?
6Au visivyoungwa huliwa pasipo chumvi? Au yako yapendezayo, ukila ute wa yai?
7Roho yangu inakataa kuvigusa tu, kwani hufanana na vyakula vyangu vichukizavyo.
8Laiti yangetimia niyatakayo, Mungu akinipa niyangojeayo!
9Kama Mungu yangempendeza, na aniponde, na aukunjue mkono wake kuikata roho yangu!
10Litakalonituliza moyo litakuwako nayo siku hiyo, ijapo niumizwe pasipo kuhurumiwa, lilo hilo litanichezesha, ndio hilo la kwamba: Sikuyakana maneno yake Mtakatifu!
11Nguvu zangu ni za nini, nitulie na kungoja? Mwisho wangu utakuwaje, nipate kuvumilia?
12Je? Kama nguvu za mawe zilivyo, ndivyo, nguvu zangu zilivyo nazo? Au mwili wangu, nilio nao, ni wa shaba?
13Je? Haya hayakunipata kwa kukosa msaada wo wote? Je? Uponya haukutoweshwa huku, niliko?
14Mwenye kuzimia hupaswa na rafiki wamwendeao kwa upole, ijapo amekwisha kuacha kumcha Mwenyezi.
15Ndugu zangu wameniacha na kudanganya kama kijito, kama mikondo ya vijito vikaukavyo upesi;[#Sh. 38:12.]
16maana hivi huwa vyeusi kwa maji ya barafu, theluji ziyeyukazo zilimoingia kujifichia humo.
17Lakini siku, vinapowakiwa na jua, hupwa, hutoweka mahali pao, kiangazi kikitimia.
18Misafara huziacha njia zao kuvipandia jangwani, lakini wasipokuta kijito chenye maji, huangamia.
19Misafara ile ya Tema huvitazamia, vikosi vya Saba huvingojea katika safari zao.[#1 Mose 25:15; Iy. 1:15.]
20Lakini huona kuwa bure kuvikimbilia, kwani wanapofika mahali pao wamedanganyika.
21Nanyi sasa mmeniwia vivyo hivyo: mlipoyaona haya mastusho mkashikwa na woga.
22Je? Nimewaambia: Nipeni? Kwa mali zenu ninyi nikomboeni?
23Au: Niponyeni mkononi mwake anisongaye, namo mikononi mwao wakorofi nikomboeni?
24Nifunzeni, nipate kunyamaza! Nitambulisheni, nilipopotea!
25Maneno yanyokayo hushinda kweli, lakini maneno yenu ya kunisuta yana maana gani?
26Je? Mwawaza mioyoni mwenu kuonya maneno tu? Maneno ya mtu azimiaye ni ya upepo tu.
27Hata mwana aliyefiwa na wazazi mwaweza kumpigia kura, mkamwuza naye aliye mwenzenu.
28Lakini sasa ninawaomba, mnielekee mimi; sitaweza kuwaongopea usoni penu.
29Rudini, msifanye upotovu! Rudini, mwone, wongofu wangu ungaliko.
30Je? Ulimi wangu umesema yaliyo mapotovu? Au kinywa changu hakiyatambui yaponzayo?