Maombolezo 1

Maombolezo 1

Yerusalemu ulio peke yake unatafuta mtuliza moyo.

1Kumbe uliokuwa mji wenye watu wengi unakaa peke yake!

Uliokuwa mkuu katika wamizimu ukawa kama mjane! Uliokuwa

mfalme wa kike wa miji unatumikishwa!

2Unalia usiku kucha, machozi yake yako mashavuni pake!

Hakuna autulizaye moyo kwao wote walioupenda,

wenziwe wote wakauacha kwa udanganyifu, wakawa adui zake.

3Wayuda wametekwa, wakapatwa na wasiwasi na utumishi

mwingi;

wanakaa kwenye wamizimu pasipo kuona kituo,

wote waliowakimbiza wakawapatia mahali pa kubanana.

4Njia za Sioni zinasikitika, kwani hakuna wajao kula

sikukuu,

malango yake yote yako peke yao, watambikaji wake

wanapiga kite,

wanawali wake wametiwa majonzi, nao wanayaona kuwa

machungu.

5Wausongao wako juu, adui zake wanafanikiwa,

kwani Bwana ameutia majonzi kwa ajili ya mapotovu yake

mengi,

wachanga wake wakatekwa na kuhamishwa mbele yao

wawasongao.

6Utukufu wake wote umemtoka yeye binti Sioni,

wakuu wake wakawa kama kulungu wasioona malisho,

wakaenda pasipo nguvu mbele yao wawakimbizao.

7Siku hizi za ukiwa na za kutangatanga Yerusalemu

unayakumbuka mema yake yote yaliyoupendeza, ambayo ulikuwa

nayo siku za kale.

Watu wake walipotiwa mkononi mwake aliyewasonga,

mwenye kuwasaidia hakuwako kabisa;

waliowasonga walipoviona, wakacheka, jinsi

walivyokomeshwa

8Yerusalemu umekosa kweli, kwa hiyo ukawa tapisho,

wote walioutukuza wakaubeza, kwani waliuona, ulipokuwa

uchi,

nao unapiga kite kwa kurudi nyuma.

9Uchafu wake umezishika nguo zake ndefu,

haukukumbuka mwisho kama huu;

hivyo ulivyobwagwa chini unastaajaabisha,

tena hakuna anayeutuliza moyo.

E Bwana, utazame ukiwa wangu! Kwani adui wanajikuza.

10Mwenye kuusonga ameukunjua mkono wake,

ayachukue mema yake yote yapendezayo;

kwani aliona wamizimu, wakipaingia Patakatifu pake,

nawe uliwakataza, wasipaingie penye mkutano wako!

11Watu wake wote wanapiga kite wakitafuta chakula,

mema yao yapendezayo wanayanunua vilaji vya kujirudisha

uzimani.

Tazama, Bwana, uone, ya kuwa ninawaziwa kuwa si kitu!

12Je? Ninyi nyote mpitao njia, haviingii mioyoni mwenu?

Chungulieni, mwone, kama yako maumivu

yaliyo sawa nayo yangu yaliyonipata mimi,

maana nimetiwa majonzi na Bwana, makali yalipomwaka

moto.

13Toka juu akatuma moto kuiingia mifupa yangu, nao

ukaishinda;

miguu yangu akaitegea tanzi, akanirudisha nyuma,

akanipa kuwa peke yangu, kwa hiyo ninaugua mchana kutwa.

14Mzigo wa mapotovu yangu ukafungwa kwa mkono wake,

yaliposhikamana yakawekwa shingoni pangu;

ndivyo, alivyozivunja nguvu zangu.

Bwana akanitia mikononi mwao, ambao siwezi kuwainukia.

15Wanguvu wangu Bwana akawatupa wote, waondoke kwangu;

akaita wengi, wanikusanyikie wawaponde wavulana wangu,

mwanamwali binti Yuda Bwana akamkanyaga kamulioni.

16Kwa hiyo ninalia machozi, macho yangu mawili

hutiririka maji,

kwani mtuza moyo anikalia mbali, ndiye awezaye kuirudisha

roho yangu.

Watoto wangu wameachwa peke yao, kwani adui wanazidi

nguvu.

17Sioni unainyosha mikono yake, lakini hakuna

anayeutuliza moyo

Bwana amewaagiza wamzungukao Yakobo, wamsonge tu;

ndipo, Yerusalemu ulipowaziwa kwao kuwa si kitu.

18Lakini Bwana ni mwongofu, kwani nalikiinukia kinywa

chake.

Yasikieni, ninyi makabila yote, kayatazameni maumivu

yangu!

Wavulana na wasichana wangu wametekwa na kuhamishwa!

19Nikawaita walionipenda, lakini wakanidanganya.

Watambikaji na wazee wangu wamezimia mijini

walipojitafutia vyakula, wazirudishe roho zao.

20Tazama, Bwana! Kwani nimesongeka: matumbo yangu

yamechafuka,

moyo wangu nao humu kifuani umepinduliwa,

kwa kuwa nalikataa kukutii kabisa.

Nje upanga unawaua watoto, nyumbani huwa kama mwake

kifo.

21Wakasikia, nilivyougua, lakini hakuna anitulizaye

moyo,

adui zangu wote walipoyasikia mabaya yaliyonipata,

wakayafurahia, ya kuwa ndiyo, uliyoyafanya wewe.

Utaileta ile siku, uliyoitangaza, ndipo, watakapokuwa

kama mimi.

22Mabaya yao yote na yatokee usoni pako,

uwafanyizie, kama ulivyonifanyizia kwa ajili ya mapotovu

yangu yote!

Kwani kupiga kite kwangu ni kwingi, nao moyo wangu huugua

tu.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania