The chat will start when you send the first message.
1Mimi ni mtu wa kiume, lakini niliteseka
nilipopigwa fimbo yenye machafuko yake.
2Akaniongoza na kuniendesha,
nije gizani, nisije mwangani.
3Ananirudia mimi peke yangu,
mkono wake ukinigeukia mchana kutwa.
4Akazinyausha nyama na ngozi za mwili wangu mimi,
mifupa yangu yote akaivunja nayo.
5Akanizibia njia
akanizungushia mambo yenye sumu na usumbufu.
6Akanikalisha penye giza kuu
kama waliokufa kale.
7Ukuta unanizunguka, nisitoke,
akanifunga minyororo mizito.
8Ijapo nilie na kupiga yowe,
maombo yangu huyazibia masikio.
9Akazifunga njia zangu kwa mawe yaliyochongwa,
napo pengine, nilipopita, akapafanya, pasipitike tena.
10Yeye akaniwia kama nyegere aoteaye
au kama simba aliomo mafichoni.
11Njia zangu akazipoteza, akaninyafua,
akaniweka mahali palipo peke yake.
12Akaupinda upindi wake, akanitumia
kuwa shabaha ya kuipiga mishale.
13Iliyokuwa podoni mwake
akaipiga, inichome mafigo
14Nikawa kicheko kwao wote walio ukoo wangu,
wakanizomea mchana kutwa.
15Akanishibisha kwa kunilisha yaumizayo matumbo,
akaninywesha maji machungu.
16Akayakerezesha meno yangu na kuyaumisha vijiwe,
akanigaagaza majivuni.
17Ukaifukuza roho yangu, isipate kutulia,
nikasahau kulivyo, mtu akikaa vema.
18Nikasema: Nguvu zangu zimepotea
pamoja na kingojeo changu cha kumngojea Bwana.
19Ukumbuke ukiwa wangu na wasiwasi wangu,
nikilishwa machungu, nikinyweshwa yenye sumu!
20Roho yangu haiachi kuyakumbuka,
kwa kuwa imeinamishwa humu ndani yangu.
21Haya na niyaweke moyoni tena,
ndivyo, nitakavyopata kumngojea:
22*Ni upole wake Bwana, tusipomalizika,
kwani huruma zake hazikuisha,
23kila kunapokucha ni mpaya,
nao walekevu wake ni mwingi.
24Fungu langu ni Bwana! ndivyo, roho yangu isemavyo:
kwa hiyo nitamngojea.
25Bwana huwawia mwema wamngojeao
nao wamtafutao kwa roho.
26Inafaa kuvumilia
na kuungojea wokovu wa Bwana.
27inamfalia mtu wa kiume,
akitwikwa mizigo akingali kijana bado.
28Na akae peke yake na kunyamaza kimya,
kwani Bwana ndiye aliyemtwika.
29kinywa chake akiweke uvumbini,
kwani labda liko la kulingojea.
30Ampigaye na amgeuzie shavu,
na ashibe matusi.
31Bwana hamtupi mtu
kale na kale.
32Bwana akimtia mtu majonzi atamhurumia tena,
kwani upole wake ni mwingi.*
33Kwani siko kupenda kwa moyo wake,
akiwaumiza wana wa watu na kuwapiga.
34Mtu akiwaponda na kuwapiga mateke kwa miguu
wote waliofungwa huku nchini,
35au mtu akimpotoa mwenziwe na kumnyima yampasayo
usoni pake Alioko huko juu,
36au mtu akimgeuza mwenziwe mkweli shaurini kuwa mwongo,
Bwana asiyatazame?
37Yuko nani awezaye kusema neno, likawapo,
Bwana asipoliagiza?
38Je? Yeye Alioko huko juu aliyoyasema,
hayatokei yakiwa mabaya au yakiwa mema?
39Mtu hununia nini siku zote za kuwapo?
Kila mtu na ayanunie makosa yake!
40Na tuzijaribu njia zetu na kuzichunguza,
tupate kurudi upande wake Bwana!
41Na tumwinulie Mungu mbinguni
mioyo yetu pamoja na mikono yetu!
42Sisi ndio tuliokosa tusipokutii,
nawe hukutuondolea.
43Ulipojivika makali ulitukimbiza,
ukaua pasipo huruma.
44Ukajivika wingu, likufunike,
malalamiko yasikufikie.
45Ukatufanya kuwa takataka za kutupwa tu
katikati ya makabila ya watu.
46Wakatuasamia vinywa vyao
wote waliokuwa adui zetu.
47Yaliyotupata yalikuwa mastuko na mashimo
na maangamizo na mavunjiko.
48Macho yangu huchuruzika vijito vya maji
kwa ajili ya mavunjiko yao walio wazaliwa wa ukoo wangu.
49Macho yangu hulia machozi
pasipo kupumzika, hayakomeki,
50mpaka Bwana achungulie toka mbinguni,
ayaone.
51Macho yangu huniumiza roho kwa kuona,
wanawake wote wa mji wangu walivyo.
52Kweli wameniwinda kama ndege
wale wanichukiao bure tu;
53wakanitupa shimoni, wanizimishe roho,
wakanitupia mawe.
54Maji yenye nguvu yakakididimiza kichwa changu,
nikasema: Basi, nimekatwa roho.
55nikalililia Jina lako, Bwana,
nilipokuwa shimoni kuzimuni.
56Ukaisikia sauti yangu nilipokuomba: Usiyazibe masikio yako,
nikikupigia kite na kukuomba wokovu.
57Ukanijia karibu siku ile, nilipokulilia,
ukaniambia: Usiogope!
58Ukanigombea magomvi ya roho yangu
ukanikomboa na kunirudisha uzimani.
59Ukaona, Bwana, jinsi nilivyopotolewa,
ukayakata mashauri yangu.
60Ukayaona yote, waliyoyataka kunilipizia,
nayo yote, waliyoyawaza ya kunifanyizia.
61Ukayasikia, Bwana, matusi yao
nayo yote, waliyoniwazia.
62Ukayasikia, waniinukiao waliyoyasema
wakinipigia mashauri mchana kutwa.
63Tazama, uone! Ikiwa wanakaa, au ikiwa wanasimama:
mimi ndiye, wanayemzomea.
64Uwalipishe, Bwana, matendo yao
ukiwafanyizia, kama mikono yao ilivyofanya!
65Uwashupaze mioyo yao,
apizo lako likiwajia!
66Uwakimbize kwa makali yako na kuwaangamiza,
watoweke chini ya mbingu za Bwana!