The chat will start when you send the first message.
1Bwana akamwambia Mose kwamba:
2Sema na wana wa Isiraeli, uchukue kwao fimbo, kwa kila mlango wa baba fimbo moja, wao wakuu wote wa milango ya baba zao wakupe fimbo 12, nawe uandike kila fimbo jina la mwenyewe.
3Nalo jina la Haroni uliandike katika fimbo ya Lawi, kwani kila fimbo moja iwe ya kichwa cha mlango wa baba zao.
4Kisha uziweke Hemani mwa Mkutano chini mbele ya Sanduku la Ushahidi hapo, ninapokutana nanyi.[#2 Mose 25:22.]
5Ndipo, fimbo yake yeye, niliyemchagua, itakapochipuka, niyakomeshe manung'uniko ya wana wa Isiraeli, wanayowanung'unikia ninyi, yasifike tena kwangu.[#4 Mose 16:5,7.]
6Mose akayaambia wana wa Isiraeli; ndipo, wakuu wao wote walipompa fimbo, kila mtu mmoja fimbo moja ya mlango wa baba zao, zikawa fimbo 12, nayo fimbo ya Haroni ilikuwa katikati yao.
7Mose akaziweka hizi fimbo mbele ya Bwana Hemani mwa Ushahidi.
8Ikawa, Mose alipoliingia Hema la Ushahidi kesho yake, akaiona fimbo yake Haroni ya mlango wa Lawi, ilikuwa imechipuka, ikachanua maua, ikazaa malozi.
9Ndipo, Mose alipozitoa hizo fimbo zote mbele ya Bwana, akazipelekea wana wa Isiraeli, nao walipoziona wakachukua kila mtu fimbo yake.
10Kisha Bwana akamwambia Mose: Irudishe fimbo ya Haroni hapo mbele ya Sanduku la Ushahidi, iwekwe kuwa kielekezo chao hawa wana wakatavu, manung'uniko yao yakome, yasifike tena kwangu, wao wasife.[#Ebr. 9:4.]
11Mose akavifanya; kama Bwana alivyomwagiza, ndivyo livyovifanya.
12Kisha wana wa Isiraeli wakamwambia Mose kwamba: Tazama, tunakufa, tunaangamia, kweli sisi sote tunaangamia.
13Kila alifikiaye Kao la Bwana, kweli kila alifikiaye karibu hufa; je? hivi hatutakwisha kufa sote? 4 Mose. 16:40.