4 Mose 26

4 Mose 26

Waisiraeli wanahesabiwa tena.

1Lile pigo lilipokwisha kukoma, Bwana akamwambia Mose na Elazari, mwana wa mtambikaji Haroni, kwamba:

2Toeni jumla yao wote walio mkutano wa wana wa Isiraeli kuanzia kwao walio wenye miaka ishirini na zaidi wa milango ya baba zao mkiwakagua wote wanaoweza kwenda vitani kwao Waisiraeli.[#4 Mose 1:2-47.]

3Kwa hiyo Mose na mtambikaji Elazari wakasema nao kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili, kwamba:

4Wahesabuni wao walio wenye miaka ishirini na zaidi, kama Bwana alivyomwagiza Mose pamoja nao wana wa Isiraeli waliotoka katika nchi ya Misri.

5Rubeni, mwana wa kwanza wa Isiraeli, wanawe Rubeni walikuwa: Henoki, baba ya ndugu zao Wahenoki, Palu, baba ya ndugu zao Wapalu;[#1 Mose 46:8-27; 1 Mambo 4—7.]

6Hesironi, baba ya ndugu zao Wahesironi, Karmi, baba ya ndugu zao Wakarmi.

7Hizi ndizo ndugu zao Warubeni, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 43730.

8Wana wa Palu walikuwa wa Eliabu;[#4 Mose 16.]

9nao hao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli na Datani na Abiramu; nao Datani na Abiramu walikuwa wale wateule wa mkutano walioshindana na Mose na Haroni katika mkutano wao wa Kora, wao waliposhindana na Bwana.

10Ilikuwa hapo, nchi ilipoasama na kuwameza pamoja na Kora; wao wa mkutano wao walipokufa, moto ulikula watu 250, wakawa kielekezo cha kutisha.

11Lakini wana wa Kora hawakufa hapo.

12Wana wa Simeoni kwa ndugu zao walikuwa: Nemueli, baba ya ndugu zao Wanemueli, Yamini, baba ya ndugu zao Wayamini, Yakini, baba ya ndugu zao Wayakini,

13Zera, baba ya ndugu zao Wazera, Sauli baba ya ndugu zao Wasauli.

14Hizi ndizo ndugu zao Wasimeoni, watu 22200.

15Wana wa Gadi kwa ndugu zao walikuwa: Sefoni, baba ya ndugu zao Wasefoni, Hagi, baba ya ndugu zao Wahagi, Suni, baba ya ndugu zao Wasuni;

16Ozini, baba ya ndugu zao Waozini, Eri, baba ya ndugu zao Waeri;

17Arodi, baba ya ndugu zao Waarodi, Areli, baba ya ndugu zao Waareli.

18Hizi ndizo ndugu zao Wagadi; nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 40500.

19Wana wa Yuda walikuwa: Eri na Onani, nao Eri na Onani walikuwa wamekufa katika nchi ya Kanaani.[#1 Mose 38:7,10.]

20Wana wa Yuda kwa ndugu zao walikuwa: Sela, baba ya ndugu zao Wasela, Peresi, baba ya ndugu zao Waperesi, Zera, baba ya ndugu zao Wazera.

21Nao wana wa Peresi walikuwa: Hesironi, baba ya ndugu zao Wahesironi, Hamuli, baba ya ndugu zao Wahamuli.[#Ruti 4:18.]

22Hizi ndizo ndugu zao Wayuda, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 76500.

23Wana wa Isakari kwa ndugu zao walikuwa: Tola, baba ya ndugu zao Watola, Puwa, baba ya ndugu zao Wapuwa;

24Yasubu, baba ya ndugu zao Wayasubu, Simuroni, baba ya ndugu zao Wasimuroni.

25Hizi ndizo ndugu zao Waisakari, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 64300.

26Wana wa Zebuluni kwa ndugu zao walikuwa: Seredi, baba ya ndugu zao Waseredi, Eloni, baba ya ndugu zao Waeloni, Yaleli, baba ya ndugu zao Wayaleli.

27Hizi ndizo ndugu zao Wazebuluni, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 60500.

28Wana wa Yosefu kwa ndugu zao walikuwa: Manase na Efuraimu.

29Wana wa Manase walikuwa: Makiri, baba ya ndugu zao Wamakiri, naye Makiri akamzaa Gileadi, naye Gileadi alikuwa baba ya ndugu zao Wagileadi.[#Yos. 17:1-3.]

30Nao wana wa Gileadi walikuwa: Iezeri, baba ya ndugu zao Waiezeri, Heleki, baba ya ndugu zao Waheleki,

31na Asirieli, baba ya ndugu zao Waasirieli, na Sekemu, baba ya ndugu zao Wasekemu,

32na Semida, baba ya ndugu zao Wasemida, na Heferi, baba ya ndugu zao Waheferi.

33Lakini Selofuhadi, mwana wa Heferi, hakuwa na mwana wa kiume, walikuwa wa kike tu, nayo majina yao hao wana wa kike wa Selofuhadi yalikuwa Mala na Noa, Hogla, Milka na Tirsa.[#4 Mose 27:10.]

34Hizi ndizo ndugu zao Wamanase, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 52700.

35Wana wa Efuraimu kwa ndugu zao walikuwa: Sutela, baba ya ndugu zao Wasutela, Bekeri, baba ya ndugu zao Wabekeri, Tahani, baba ya ndugu zao Watahani.

36Nao hawa walikuwa wana wa Sutela: Erani, baba ya ndugu zao Waerani.

37Hizi ndizo ndugu zao wana wa Efuraimu, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 32500. Hawa walikuwa wana wa Yosefu kwa ndugu zao.

38Wana wa Benyamini kwa ndugu zao walikuwa: Bela, baba ya ndugu zao Wabela, Asibeli, baba ya ndugu zao Waasibeli, Ahiramu, baba ya ndugu zao Waahiramu,

39Sufamu, baba ya ndugu zao Wasufamu, Hufamu, baba ya ndugu zao Wahufamu.

40Nao wana wa Bela walikuwa Ardi na Namani, baba ya ndugu zao Waardi na baba ya ndugu zao Wanamani.

41Hawa walikuwa wana wa Benyamini kwa ndugu zao, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 45600.

42Hawa walikuwa wana wa Dani kwa ndugu zao: Suhamu, baba ya ndugu zao Wasuhamu; hizi ndizo ndugu zao Wadani kwa ndugu zao.

43Nao wa kwao ndugu zao Wasuhamu waliokaguliwa walikuwa watu 64400.

44Wana wa Aseri kwa ndugu zao walikuwa: Imuna, baba ya ndugu zao Waimuna, Iswi, baba ya ndugu zao Waiswi, Beria, baba ya ndugu zao Waberia.

45Wana wa Beria walikuwa: Heberi, baba ya ndugu zao Waheberi, Malkieli, baba ya ndugu zao Wamalkieli.

46Nalo jina la mwanawe wa kike wa Aseri alikuwa Sara.

47Hizi ndizo ndugu zao wana wa Aseri, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 53400.

48Wana wa Nafutali kwa ndugu zao walikuwa: Yaseli, baba ya ndugu zao Wayaseli, Guni, baba ya ndugu zao Waguni,

49Yeseri, baba ya ndugu zao Wayeseri, Silemu, baba ya ndugu zao Wasilemu.

50Hizi ndizo ndugu zao Wanafutali kwa ndugu zao; nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 45400.

51Hii ilikuwa jumla ya wana wa Isiraeli waliokaguliwa watu 601730.

52Kisha Bwana akamwambia Mose kwamba:

53Hawa ndio watakaogawiwa nchi hiyo kwa hesabu ya majina.

54Walio wengi uwagawie fungu kubwa zaidi kuwa lao, nao walio wachache uwagawie fungu lililo dogo kidogo kuwa lao; kila shina sharti lipate fungu lake kwa hesabu yao waliokaguliwa kwake.

55Lakini nchi sharti igawanywe kwa kupiga kura, wapate mafungu yao kwa majina ya baba za mashina.[#4 Mose 33:54; Yos. 14:2.]

56Wao walio wengi nao walio wachache sharti mafungu yao ya kuwa yao wenyewe wagawiwe kwa kupigiwa kura.

57Nayo hii ndiyo jumla ya Walawi kwa ndugu zao: Gersoni, baba ya ndugu zao Wagersoni, Kehati, baba ya ndugu zao Wakehati, Merari baba ya ndugu zao Wamerari.[#2 Mose 6:16-25.]

58Hizi ndizo ndugu zao Walawi: Ndugu zao Walibuni, ndugu zao Waheburoni, ndugu zao Wamahali, ndugu zao Wamusi, ndugu zao Wakora. Naye Kehati alimzaa Amuramu.

59Nalo jina lake mkewe Amuramu alikuwa Yokebedi, binti Lawi, huyu Lawi aliyezaliwa huko Misri, naye akamzalia Amuramu Haroni na Mose na umbu lao Miriamu.

60Naye Haroni aliwazaa: Nadabu na Abihu na Elazari na Itamari.

61Lakini Nadabu na Abihu walikufa walipomtolea Bwana ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa isiyopasa.[#3 Mose 10:1-2.]

62Jumla yao ilikuwa watu 23000, ndio wa kiume wote waliokuwa wenye mwezi mmoja na zaidi; kwani hawakukaguliwa katikati ya wana wa Isiraeli, kwa kuwa hawakupewa fungu lao wenyewe katikati ya wana wa Isiraeli.

63Hii ndiyo jumla yao, Mose na mtambikaji Elazari waliowakagua, walipowakagua wana wa Isiraeli kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili.

64Miongoni mwao hakuwamo mtu hata mmoja wao, Mose na mtambikaji Haroni waliowakagua walipowakagua wana wa Isiraeli nyikani kwa Sinai.[#4 Mose 3:1-39.]

65Kwani Bwana aliwaambia: Hamna budi kufa nyikani; kwa hiyo hakusalia mtu hata mmoja kwao, ni Kalebu tu, mwana wa Yefune, na Yosua, mwana wa Nuni.[#4 Mose 14:22-38.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania