The chat will start when you send the first message.
1Wakaja wana wa kike wa Selofuhadi, mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, waliokuwa wa ndugu za Manase, mwana wa Yosefu, majina yao hawa wanawe wa kike ndiyo haya: Mala na Noa na Hogla na Milka na Tirsa.[#4 Mose 26:33; 36:2; Yos. 17:3-6.]
2Hao wakamtokea Mose na mtambikaji Elazari na wakuu wa mkutano wote hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, wakasema:
3Baba yetu alikufa nyikani, naye hakuwa katika mkutano wao waliofanya shauri la kumpingia Bwana katika mkutano wao Wakora, ila alikufa kwa ukosaji wake yeye, lakini hakuwa na wana wa kiume.[#4 Mose 16:2; 26:65.]
4Mbona jina la baba yetu litoweke katika ndugu zake, kwa kuwa hakuwa na mwana wa kiume? Tupe sisi fungu katikati ya ndugu za baba yetu, tulichukue!
5Mose akalitokeza hilo shauri lao mbele ya Bwana.[#3 Mose 24:12.]
6Naye Bwana akamwambia Mose kwamba:
7Haya, wana wa kike wa Selofuhadi waliyoyasema, ndiyo ya kweli. Uwape katikati ya ndugu za baba yao fungu, walichukue, liwe lao, ukiagiza, fungu la baba yao walipate wao.
8Nao wana wa Isiraeli waambie kwamba: Mtu akifa pasipo kuwa na mwana wa kiume, fungu lake huyu sharti mmwachie mwanawe wa kike.
9Kama hata mwana wa kike hakuwa naye, mtawapa ndugu zake fungu lake.
10Kama hata ndugu hakuwa nao, mtawapa ndugu za baba yake fungu lake.
11Kama baba yake hakuwa na ndugu, basi, hilo fungu lake mtampa ye yote aliye ndugu yake wa kuzaliwa naye wa mlango wake, alichukue. Haya na yawe kwao wana wa Isiraeli maongozi yenye haki, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
12Bwana akamwambia Mose: Panda huku juu mlimani kwa Abarimu, uitazame hiyo nchi, nitakayowapa wana wa Isiraeli.[#5 Mose 32:48-49.]
13Ukiisha kuiona utachukuliwa nawe kwenda kwao walio ukoo wako, kama kaka yako Haroni alivyochukuliwa naye kwenda huko.[#4 Mose 20:24,28.]
14Ni kwa kuwa nyikani kwa Sini hamkukitii vema kinywa changu cha kwamba: Mnitakase kwa kutoa maji machoni pao, mkutano huu uliponigombeza; hayo yalikuwa penye Maji ya Magomvi kule Kadesi nyikani kwa Sini.[#4 Mose 20:12-13.]
15Naye Mose akamwambia Bwana kwamba:
16Bwana wangu aliye mwenye roho zao wote walio wenye miili na aweke mtu kuwa mkuu wa mkutano huu,[#4 Mose 16:22.]
17atakayewatangulia kwa kutoka na kuingia kwake, atakayewaongoza wao, wapate kutoka na kuingia tena, watu wa mkutano huu wa Bwana wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji.[#Mat. 9:36.]
18Ndipo, Bwana alipomwambia Mose: Mchukue Yosua, mwana wa Nuni, aliye mtu mwenye Roho yangu moyoni mwake, umbandikie mkono kichwani pake![#5 Mose 3:21; 34:9.]
19Kisha msimamishe mbele ya mtambikaji Elazari machoni pao walio wa mkutano huu, umwagizie mambo yako machoni pao
20na kumgawia utukufu wako, umkalie naye, watu wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli wamsikie.[#2 Fal. 2:9,15.]
21Itakapotukia, na amtokee mtambikaji Elazari, ampigie bao na kuutumia Urimu mbele ya Bwana, kama desturi; utakaposema, watoke, sharti watoke, tena utakaposema, waingie, sharti waingie, yeye na wana wote wa Isiraeli pamoja naye, huo mkutano wote pia.[#2 Mose 28:30.]
22Mose akafanya, kama Bwana alivyomwagiza: akamchukua Yosua, akamsimamisha mbele ya mtambikaji Elazari na mbele ya mkutano wote.
23Kisha akambandikia mikono yake kichwani pake, akamwagizia mambo yake, kama Bwana alivyosema kinywani mwa Mose.