The chat will start when you send the first message.
1Bwana akamwambia Mose kwamba:[#3 Mose 21:6.]
2Waagize wana wa Isiraeli, uwaambie: Jiangalieni, mnitolee wakati huo uliowekwa matoleo yanayonipasa, ndio chakula changu cha ng'ombe za tambiko zinazoteketezwa kuwa mnuko wa kunipendeza.
3Uwaambie: Nazo hizi ndizo ng'ombe za tambiko za kuteketezwa, mtakazomtolea Bwana: Wana kondoo wa mwaka mmoja wasio na kilema, pasipo kukoma kila siku wawili kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima.[#2 Mose 29:38-42.]
4Mwana kondoo mmoja utamtoa asubuhi, naye mwana kondoo wa pili utamtoa saa za jioni.
5Pamoja naye utoe vibaba vitatu vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na kibaba kimoja cha mafuta yaliyotwangwa vema kuwa kilaji cha tambiko.[#3 Mose 2:1.]
6Hii ndio ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima iliyotolewa kila siku mlimani kwa Sinai kuwa moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
7Tena utoe kinywaji chake cha tambiko, kibaba kimoja cha mvinyo kwa kila mwana kondoo, nacho hicho kinywaji cha tambiko cha mvinyo yenye nguvu ummiminie Bwana hapo Patakatifu.
8Naye mwana kondoo wa pili na umtoe saa za jioni pamoja na kilaji cha tambiko na kinywaji chake cha tambiko kama asubuhi; ukifanya hivyo, vitakuwa moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
9Tena siku ya mapumziko mtoe wana kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na kilema na vibaba sita vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko, tena kinywaji chake cha tambiko.[#Mat. 12:5.]
10Hizi ndizo ng'ombe za tambiko za kila siku ya mapumziko, mtakazozitoa pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kila siku na kinywaji chake cha tambiko.
11Tena siku za kwanza za miezi yenu na mmtolee Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima: madume mawili ya ng'ombe walio vijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema.[#4 Mose 10:10.]
12Tena mtoe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko cha dume moja la ng'ombe na vibaba sita vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko cha dume moja la kondoo.[#4 Mose 15:2-13; 28:20,28.]
13Tena vibaba vitatutatu vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko cha kila mwana kondoo mmoja. Ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima itakayotolewa hivyo itakuwa moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
14Navyo vinywaji vyao vya tambiko na viwe vibaba viwili vya mvinyo vya dume moja la ng'ombe na kibaba kimoja na nusu cha mvinyo cha dume la kondoo na kibaba kimoja cha mvinyo cha mwana kondoo mmoja. Hizi ndizo ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima za mwandamo wa mwezi, mtakazozitoa mwezi kwa mwezi mwaka mzima.
15Tena pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku Bwana na atolewe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na kinywaji chake cha tambiko.[#4 Mose 28:22.]
16Siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza ni Pasaka ya Bwana.[#3 Mose 23:5-14.]
17Siku ya kumi na tano ya mwezi huo na mle sikukuu; ndipo iliwe mikate isiyochachwa siku saba.
18Siku ya kwanza na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi,[#4 Mose 28:25-26.]
19ila mmtolee Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima motoni: madume mawili ya ng'ombe walio vijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema; hawa ndio, mtakaowatoa.
20Navyo vilaji vyao vya tambiko na mtoe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume moja la ng'ombe na vibaba sita vya dume la kondoo.[#4 Mose 28:12.]
21Tena na mtoe vibaba vitatutatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo saba.
22Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo kuwapatia ninyi upozi.[#4 Mose 28:15.]
23Hao sharti mwatoe pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya asubuhi inayotolewa kila siku.
24Hao na mwatoe kila siku siku hizo saba kuwa chakula cha moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana; nao na watolewe pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na kinywaji chake cha tambiko.
25Siku ya saba na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi.
26Siku ya malimbuko, mtakapomtolea Bwana vilaji vipya vya tambiko, ndio sikukuu yenu ya majuma saba; hapo na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi.[#3 Mose 23:15-21.]
27Tena na mtoe kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe mnuko wa kumpendeza Bwana: madume mawili ya ng'ombe walio vijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja.
28Navyo vilaji vyao vya tambiko na viwe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume moja la ng'ombe na vibaba sita vya dume moja la kondoo,
29tena vibaba vitatutatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo saba.
30Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwapatia ninyi upozi.[#4 Mose 28:15.]
31Hao na mwatoe pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na kilaji chake cha tambiko; nao sharti wawe pasipo kilema, tena mtoe navyo vinywaji vyao vya tambiko.