4 Mose 33

4 Mose 33

Makambi ya Waisiraeli.

1Hizi ndizo safari za wana wa Isiraeli, vikosi vyao vilipotoka katika nchi ya Misri, wakiongozwa na Mose na Haroni.

2Mose akaziandika hizo safari zao, kama walivyotoka na kuondoka kwa kuagizwa na Bwana, nayo haya ndiyo matuo yao, walipoondoka kwendelea katika safari zao:

3siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, ndiyo siku ya pili ya Pasaka, ndipo, wana wa Isiraeli walipoondoka Ramusesi machoni pao Wamisri wote kwa nguvu za mkono uliotoka juu.[#2 Mose 1:11; 14:8.]

4Nao Wamisri walikuwa wakiwazika wana wao wote wa kwanza, Bwana aliowapiga kwao, kwani Bwana aliihukumu miungu yao.[#2 Mose 12:12.]

5Wana wa Isiraeli walipoondoka Ramusesi wakapiga makambi Sukoti.[#2 Mose 12:37.]

6Walipoondoka sukoti wakapiga makambi Etamu ulioko kwenye mapeo ya nyika.[#2 Mose 13:20.]

7Walipoondoka Etamu wakarudi Pi-Hahiroti unaoelekea Baali-Sefoni, wakapiga makambi mbele ya Migidoli.[#2 Mose 14:2.]

8Walipoondoka mbele yake Hahiroti wakapita katikati ya bahari, wakaingia nyikani; walipokwenda safari ya siku tatu katika nyika ya Etamu wakapiga makambi Mara.[#2 Mose 14:22; 15:23.]

9Walipoondoka Mara wakafika Elimu; nako huko Elimu kulikuwa na visima vya maji 12 na mitende 70; kwa hiyo walipiga makambi huko.[#2 Mose 15:27.]

10Waalipondoka Elimu wakapiga makambi kwenye Bahari Nyekundu.

11Walipoondoka kwenye Bahari Nyekundu wakapiga makambi nyikani kwa Sini.[#2 Mose 16:1.]

12Walipoondoka nyikani kwa Sini wakapiga makambi Dofuka.

13Walipoondoka Dofuka wakapiga makambi Alusi.

14Walipoondoka Alusi wakapiga makambi Refidimu; huko ndiko, watu walikokosa maji ya kunywa.[#2 Mose 17:1.]

15Walipoondoka Refidumu wakapiga makambi nyikani kwa Sinai.[#2 Mose 19:1.]

16Walipoondoka nyikani kwa Sinai wakapiga makambi kwenye Makaburi ya Uchu.[#4 Mose 11:34.]

17Walipoondoka kwenye Makaburi ya Uchu, wakapiga makambi Haseroti.[#4 Mose 11:35.]

18Walipoondoka Haseroti wakapiga makambi Ritima.[#4 Mose 12:16.]

19Walipoondoka Ritima wakapiga makambi Rimoni-Peresi.

20Walipoondoka Rimoni-Peresi wakapiga makambi Libuna.

21Walipoondoka Libuna wakapiga makambi Risa.

22Walipoondoka Risa wakapiga makambi Kehelata.

23Walipoondoka Kehelata wakapiga makambi mlimani kwa Seferi.

24Walipoondoka mlimani kwa Seferi wakapiga makambi Harada.

25Walipoondoka harada wakapiga makambi Makeloti.

26Walipoondoka Makeloti wakapiga makambi Tahati.

27Walipoondoka Tahati wakapiga makambi Tara.

28Walipoondoka Tara wakapiga makambi Mitika.

29Walipoondoka Mitika wakapiga makambi Hasimona.

30Walipoondoka Hasimona wakapiga makambi Moseroti.

31Walipoondoka Moseroti wakapiga makambi kwa wana wa Yakani.[#5 Mose 10:6.]

32Walipoondoka kwa wana wa Yakani wakapiga makambi Hori-Hagidigadi.

33Walipoondoka Hori-Hagidigadi wakapiga makambi Yotibata.[#5 Mose 10:7.]

34Walipoondoka Yotibata wakapiga makambi Aburona.

35Walipoondoka Aburona wakapiga makambi Esioni-Geberi.[#4 Mose 20:1.]

36Walipoondoka Esioni-Geberi wakapiga makambi nyikani kwa Sini, ndio Kadesi.

37Walipoondoka Kadesi wakapiga makambi mlimani kwa Hori kwenye mwisho wa nchi ya Edomu.[#4 Mose 20:22-29.]

38Ndipo, mtambikaji Haroni alipopanda mlimani kwa Hori kwa kuagizwa na Bwana, akafa huko siku ya kwanza ya mwezi wa tano katika mwaka wa arobaini tangu hapo, wana wa Isiraeli walipotoka katika nchi ya Misri;

39naye alikuwa mwenye miaka 123, alipokufa mlimani kwa Hori.

40Ndipo, Aradi, mfalme wa Kanaani, aliposikia, ya kuwa wana wa Isiraeli wanakuja; maana alikaa upande wa kusini wa nchi ya Kanaani.[#4 Mose 21:1.]

41Walipoondoka mlimani kwa Hori wakapiga makambi Salmona.

42Walipoondoka Salmona wakapiga makambi Punoni.

43Walipoondoka Punoni wakapiga makambi Oboti.[#4 Mose 21:10.]

44Walipoondoka Oboti wakapiga makambi Iye-Abarimu mpakani kwa Moabu.[#4 Mose 21:11.]

45Walipoondoka huko Iyimu wakapiga makambi Diboni wa Gadi.

46Walipoondoka Diboni wa Gadi wakapiga makambi Almoni-Dibulataimu.

47Walipoondoka Almoni-Dibulataimu wakapiga makambi milimani kwa Abarimu kunakoelekea Nebo.[#4 Mose 21:20.]

48Walipoondoka milimani kwa Abarimu wakapiga makambi kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili.[#4 Mose 22:1; 5 Mose 32:49.]

49Huko Yordani ndiko, walikopiga makambi kutoka Beti-Yesimoti mpaka Abeli-Sitimu kwenye mbuga za Moabu.[#4 Mose 25:1.]

Waisiraeli wanaagizwa kuwaangamiza Wakanaani.

50Bwana akamwambia Mose huko kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili, kwamba:

51Sema na wana wa Isiraeli, uwaambie: Mtakapouvuka Yordani kuingia katika nchi ya Kanaani.

52sharti mwafukuze mbele yenu wenyeji wote wa nchi hiyo, kisha myaharibu mawe yao yote yenye machorochoro ya kuyaangukia, navyo vinyago vyao vyote vilivyoyeyushwa sharti mviharibu, napo pao pote pa kutambikia vilimani sharti mpabomoe.

53Kisha mtaichukua hiyo nchi, mkae huko, kwani nimewapa ninyi nchi hiyo, mwichukue, iwe yenu.

54Nayo nchi mtaigawanyia ndugu zenu kwa kupiga kura; ndugu walio wengi mwagawie fungu kubwa zaidi kuwa lao, nao walio wachache mwagawie fungu lililo dogo kidogo kuwa lao. Huko, kura itakakomwangukia kila mtu, kutakuwa kwake; sharti mgawiane mafungu yenu kwa mashina ya baba zao.[#4 Mose 26:55.]

55Lakini msipowafukuza mbele yenu wenyeji wa nchi hiyo, basi, hao mtakaowasaza watakuwa miiba machoni penu na machomo mbavuni penu, wawasonge ninyi katika nchi, mtakayoikaa ninyi.[#Yos. 23:13.]

56Mwisho utakuwa, niwafanyizie ninyi yaleyale, niliyoyawaza kuwafanyizia wao.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania