The chat will start when you send the first message.
1Bwana akamwambia Mose kwamba:[#2 Mose 23:31.]
2Waagize wana wa Isiraeli, uwaambie: Mtakapoingia katika nchi ya Kanaani, basi, nchi itakayowaangukia kuwa fungu lenu itakuwa nchi ya Kanaani hivyo, ilivyo na mipaka yake.
3Mpaka wenu wa kusini utoke nyikani kwa Sini, uendelee kando ya Edomu; hivyo mpaka wenu wa kusini utaanzia upande wa maawioni kwa jua kwenye mwisho wa Bahari ya Chumvi.[#Yos. 15:1.]
4Kisha huo mpaka upazungukie hapo pa kukwelea Akarabimu upande wake wa kusini, kisha upitie sini, utokee upande wa kusini wa Kadesi-Barnea, kisha utokee kwenye ua wa Adari na kufikia Asimoni.
5Kutoka Asimoni mpaka ukigeukie kijito cha Misri, upate kutokea baharini.
6Mpaka wenu wa upande wa baharini utakuwa Bahari Kubwa; huu utakuwa mpaka wenu wa upande wa baharini.
7Mpaka wenu wa kaskazini utoke kwenye Bahari Kubwa, mwufikishe mlimani kwa Hori;
8toka mlimani kwa Hori mwufikishe mpaka Hamati, kisha mpaka huu tokee Sedadi.
9Ukitoka hapo, mpaka uendelee kufika Zifuroni, kisha utokee kwenye ua wa Enani. Huu utakuwa mpaka wenu wa kaskazini.
10Mpaka wenu wa upande wa maawioni kwa jua utoke kwenye ua wa Enani, mwufikishe Sefamu;
11toka Sefamu mpaka na utelemkie Ribula na kupita Aini upande wa maawioni kwa jua; kisha mpaka uendelee kutelemka, hata ufike kando ya bahari ya Kinereti upande wake wa maawioni kwa jua.[#Luk. 5:1.]
12Kisha mpaka wa utelemke na kuufuata mto na Yordani, hata utokee kwenye Bahari ya Chumvi. Hii itakuwa nchi yenu yenye hiyo mipaka yake inayoizunguka pande zote.
13Kisha Mose akawaagiza wana wa Isiraeli kwamba: Hiyo ndiyo nchi, mtakayoipata kwa kupiga kura, mwichukue, iwe yenu, naye Bwana ameagiza kuipa yale mashina tisa na nusu ya Manase.
14Kwani wao wa shina la Rubeni wamekwisha kuipatia milango ya baba zao, nao wa shina la wana wa Gadi wamekwisha kuipatia milango ya baba zao, nao walio nusu ya shina la Manase wamekwisha kujipatia mafungu yao.[#4 Mose 32:33.]
15Hayo mashina mawili na nusu ya shina la Manase wamekwisha kujipatia mafungu yao ng'ambo ya Yordani ya mashariki iliyo ya maawioni kwa jua, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili.
16Kisha Bwana akamwambia Mose kwamba:
17Haya ndiyo majina ya watu watakaowagawanyia ninyi nchi hiyo, iwe yenu: mtambikaji Elazari na Yosua, mwana wa Nuni.[#5 Mose 1:38; Yos. 14:1; 21:1.]
18Tena sharti mchukue mkuu mmoja mmoja wa kila shina moja wa kusaidia kuigawanya nchi hiyo.
19Nayo haya ndiyo majina ya watu hao: wa shina la Yuda Kalebu, mwana wa Yefune.[#4 Mose 13:6,30.]
20Wa shina la wana wa Simeoni Samueli, mwana wa Amihudi.
21Wa shina la Benyamini Elidadi, mwana wa Kisiloni.
22Wa shina la wana wa Dani mkuu Buki, mwana wa Yogli.
23Wa wana wa Yosefu: wa shina la wana wa Manase mkuu Hanieli, mwana wa Efodi.
24Wa shina la wana wa Efuraimu mkuu Kemueli, mwana wa Sifutani.
25Wa shina la wana wa Zebuluni mkuu Elisafani, mwana wa Parnaki.
26Wa shina la wana wa Isakari mkuu Paltieli, mwana wa Azani.
27Wa shina la wana wa Aseri mkuu Ahihudi, mwana wa Selomi.
28Wa shina la wana wa Nafutali mkuu Pedaheli, mwana wa Amihudi.
29Hawa ndio, Bwana aliowaagiza, kuwagawanyia wana wa Isiraeli mafungu yao katika nchi ya Kanaani.