The chat will start when you send the first message.
1Bwana akamwambia Mose kwamba:[#2 Mose 25:31-40.]
2Sema na Haroni na kuwambia: Utakapoziweka taa juu ya kinara, uangalie, hizi taa zote saba ziangaze mahali pale palipo mbele ya kinara.
3Haroni akafnya hivyo; alipoziweka hizo taa, huangalia, ziangaze mahali palipo mbele ya kinara, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
4Nacho kinara kilikuwa kimetengenezwa kwa kufua dhahabu; toka shina lake hata maua yake, yote pia ilikuwa kazi ya kufuafua dhahabu; kama ule mfano ulivyokuwa, Bwana aliomwonyesha Mose, ndivyo, walivyokitengeneza hicho kinara.
5Bwana akamwambia Mose kwamba:[#Mal. 3:3.]
6Wachukue Walawi na kuwatoa katikati ya wana wa Isiraeli, upate kuwatakasa.
7Nawe uwafanyizie hivyo ukiwatakasa: wanyunyizie maji ya weuo, nao na wajinyoe kwa wembe miili yao yote mizima, kisha na wazifue nguo zao, wapate kutakata.[#4 Mose 5:17; 19:9-17; 3 Mose 14:8.]
8Kisha na wachukue dume la ng'ombe aliye kijana bado pamoja na kilaji chake cha tambiko, ndio unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta. Nawe uchukue dume jingine la ng'ombe aliye kijana bado kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.
9Kisha wapeleke Walawi, wafike mbele ya Hema la Mkutano, ukiwakusanya nao wote walio wa mkutano wa wana wa Isiraeli.
10Kisha watokeze Walawi usoni pa Bwana, wana wa Isiraeli wakiwabandikia Walawi mikono yao.
11Naye Haroni na awapitishe Walawi mbele ya Bwana huku na huko, wawe kipaji cha tambiko, wana wa Isiraeli walichokitoa cha kupitishwa motoni mbele ya Bwana, wapate kuutumikia utumishi wa Bwana.[#4 Mose 8:21.]
12Kisha Walawi na waibandike mikono yao vichwani pao wale ng'ombe, kisha umtumie mmoja kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo, wa pili kuwa ng'ombe ya tambiko ya Bwana ya kuteketezwa nzima, uwapatie Walawi upozi.
13Kisha wasimamishe Walawi mbele ya Haroni na mabele ya wanawe na kuwapitishwa mbele ya Bwana huku na huko, wawe kipaji cha tambiko cha kupitishwa motoni.
14Ndivyo, utakavyowatenga Walawi na kuwatoa katikati ya wana wa Isiraeli, Walawi wapate kuwa wangu.[#4 Mose 3:45.]
15Baadaye Walawi na waingie kulitumikia Hema la Mkutano. Hivyo ndivyo, utakavyowatakasa na kuwapitisha huku na huko mbele ya Bwana, wawe kipaji cha tambiko cha kupitishwa motoni.
16Kwani hawa ndio niliopewa, watolewe katikati ya wana wa Isiraeli kuwa makombozi ya watoto wote wa kiume watakaozaliwa wa kwanza na mama zao; mahali pao hao wana wote wa kwanza nimewachukua wao kwa wana wa Isiraeli kuwa wangu.[#4 Mose 3:12.]
17Kwani kila mwana wa kwanza kwao wana wa Isiraeli ni wangu, kama ni wa mtu au wa nyama wa kufuga tangu siku ile, nilipowapiga wana wa kwanza wote katika nchi ya Misri; ndivyo, nilivyowatakasa, wawe wangu,[#2 Mose 13:2.]
18nikiwachukua Walawi kuwa makombozi ya wana wote wa kwanza kwao wana wa Isiraeli.
19Nami hawa Walawi nikiwapa Haroni na wanawe, wawe kipaji chao kilichotolewa katikati yao wana wa Isiraeli, wautumikie utumishi wao wana wa Isiraeli wa Hemani mwa Mkutano na kuwapatia wana wa Isiraeli upozi, hao wana wa Isiraeli wasipatwe na pigo lo lote, wao wana wa Isiraeli wakilikaribia Hema la Mkutano.
20Kwa hiyo Mose na Haroni nao wote waliokuwa wa mkutano wa wana wa Isiraeli wakawafanyizia Walawi yote sawasawa, kama Bwana alivyomwagiza Mose kuwafanyizia Walawi; hivyo ndivyo, wana wa Isiraeli walivyowafanyizia.
21Walawi walipokwisha kujieua na kuzifua nguo zao, Haroni akawapitisha huku na huko mbele ya Bwana, kisha Haroni akawapatia upozi kwa hivyo, alivyowatakasa.[#4 Mose 8:11.]
22Baadaye Walawi wakaingia kuutumikia utumishi wa Hemani mwa Mkutano machoni pa Haroni napo machoni pa wanawe; kama Bwana alivyomwagiza Mose kuwafanyizia Walawi, ndivyo, walivyowafanyizia.
23Bwana akamwambia Mose kwamba:
24Hii ndiyo inayowapasa Walawi: tangu hapo, mtu alipopata miaka 25 na zaidi na aingie zamu ya utumishi wa Hemani mwa Mkutano.[#4 Mose 4:3,23,30,47.]
25Lakini tangu hapo, mtu anapopata miaka 50 na atoke katika zamu ya utumishi huo, asiutumikie tena.
26Wataweza kuwasaidia ndugu zao mle Hemani mwa Mkutano na kulinda ulinzi, lakini kazi za utumishi wasizifanye. Hivyo ndivyo, utakavyowafanyizia Walawi, waziangalie kazi zao.