The chat will start when you send the first message.
1Bwana ndiye, nimkimbiliaye, nanyi mnaiambiaje roho yangu: Rukia mlimani kama ndege?[#1 Sam. 26:20.]
2Kwani watazameni wasiomcha Mungu, wanapinda pindi, wakapachika mishale penye upote, wapige gizani wanyokao mioyo.[#Sh. 37:14; 64:4-5.]
3Misingi inapobomolewa, mwongofu atafanyaje?
4Bwana yumo Jumbani mwake mwenye utakatifu, yeye Bwana kiti chake cha uamuzi kiko mbinguni, macho yake huwachungulia wana wa watu, kope zake ziwajaribu.[#Sh. 33:13-14; Yes. 66:1; Hab. 2:20.]
5Bwana humjaribu naye mwongofu, roho yake humchukia asiyemcha naye apendaye ukorofi.[#Sh. 5:5.]
6Atawanyeshea matanzi wao wasiomcha, tena mvua za moto na za viberitiberiti, nao upepo wa kuchoma moto ndio kinywaji, watakachogawiwa.[#1 Mose 19:24.]
7Kwani Bwana ni mwongofu, hupenda yaongokayo; kwa hiyo anyokaye moyo atauona uso wake.[#Sh. 17:15; 33:5; Mat. 5:8.]