The chat will start when you send the first message.
1Bwana asipoijenga nyumba, waijengao hujisumbua bure; Bwana asipoulinda mji, walinzi huwa macho bure.
2Ni bure mkijidamka mapema, tena mkichwelewa kazini, mkala chakula wenye machungu yasiyokoma mioyoni; kwani wamchao huwapa, wakiwa wamelala usingizi.[#Fano. 10:22.]
3Tazameni: Watoto ndio tunzo, Bwana ampatialo mtu, nao uzao wa tumbo ni kipaji chake.[#1 Mose 33:5; Sh. 128:3-4.]
4Kama mishale ilivyo katika mkono wa mpiga vita. ndivyo, wana wa kiume walivyo, wakiwa wenye nguvu za ujana.
5Mwenye shangwe ni mpiga vita aliyelijaza podo lake hao, hawa hawatatwezeka wakisemeana nao adui zao malangoni.[#Amo. 5:15.]