Mashangilio 131

Mashangilio 131

Utulivu wa moyo.

1Bwana, moyo wangu haujikuzi, wala macho yangu hayatazami juu, wala sifuatii makuu na mataajabu yanishindayo nguvu,[#Rom. 12:16.]

2lakini nimeituliza roho yangu, nikainyamazisha. Kama mtoto anavyotulia kifuani kwa mama yake akiisha kuzoezwa, asinyonye tena, ndivyo, roho yangu inavyotulia kifuani mwangu, ikiwa kama mtoto aliyezoezwa hivyo.

3Waisiraeli na wamngoje bwana kuanzia sasa hata kale na kale![#Sh. 130:7.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania