Mashangilio 132

Mashangilio 132

Kuuombea Sioni.

1Bwana, mkumbukie Dawidi masumbuko yake yote!

2Yeye alimwapia Bwana, kisha akamwagia naye yule Mwenye nguvu aliye Mungu wa Yakobo:[#2 Sam. 7.]

3Sitaingia nyumbani mwangu, nilimotua, wala sitapanda kitandani pangu pa kulalia,

4nitayazuia macho yangu, yasipate uzingizi, nitaziangalia nazo kope zangu, zisisinzie,

5mpaka nitakapompatia Bwana mahali pa kuwapo, pawe makao yake Mwenye nguvu aliye Mungu wa Yakobo.[#Tume. 7:46.]

6Ndivyo, tulivyovisikia katika nchi ya Efurata, ndivyo, tulivyoviona mashambani kwenye misitu.[#1 Sam. 7:1; 2 Sam. 6:3.]

7Na tuingie hapo, makao yake yalipo! Na tumwangukie hapo, anapowekea miguu yake!

8Inuka, Bwana, uingie penya kituo chako, wewe na Sanduku la Agano lenye nguvu zako,[#4 Mose 10:35; 2 Mambo 6:41-42.]

9watambikaji wako wajivike wongofu, wakuchao washangilie!

10Kwa ajili ya mtumishi wako Dawidi usiurudishe nyuma uso wake yeye, uliyempaka mafuta.

11Bwana alimwapia Dawidi kiapo cha kweli, naye hatakiacha akirudi nyuma:[#Sh. 89:4.]

12Walio uzao wa mwili wako nitawaketisha katika kiti chako cha kifalme, Kama wanao watalishika Agano langu, walifanye, kama watayashika hayo mashuhuda yangu, nitakayowafundisha, wana wao wataketi kale na kale katika kiti chako cha kifalme.

13Kwani Bwana aliuchagua mji wa Sioni, akaupenda, uwe Kao lake:[#Sh. 68:17; 76:3.]

14Hapo ndipo, kitakapokuwa kituo changu cha kale na kale, hapo ndipo, nitakapokaa, kwani nimepapenda.

15Vilaji vyake nitavibariki, nao maskini wake nitawashibisha mikate.

16Watambikaji wake nitawavika wokovu, nao wanichao watapiga vigelegele.

17Hapo ndipo, nitakapolivumisha baragumu lake Dawidi, limpatie nguvu, naye, niliyempaka mafuta, nitamtengenezea taa.[#Sh. 89:25; 2 Sam. 7:16; Luk. 1:69.]

18Walio adui zake nitawavika soni, lakini kichwani pake kitametameta kilemba, nilichomfunga.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania