The chat will start when you send the first message.
1Mshukuruni Bwana, ya kuwa ni mwema, ya kuwa upole wake ni wa kale na kale![#Sh. 106:1.]
2Mshukuruni Mungu, aipitaye miungu,
ya kuwa upole wake ni wa kale na kale!
3Mshukuruni Bwana wa mabwana,
ya kuwa upole wake ni wa kale na kale!
4Ni yeye peke yake afanyaye mataajabu makuu,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
5Ndiye aliyezifanya mbingu kwa utambuzi wake,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
6Ndiye aliyeitandika nchi juu ya maji,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
7Ndiye aliyeifanya mianga mikubwa,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
8Jua alilipa kutawala mchana,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
9Mwezi pamoja na nyota alizipa kutawala usiku,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
10Ndiye aliyewapiga wazaliwa wa kwanza kule Misri,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
11Akawatoa Waisiraeli katika nchi yao,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
12Kwa nguvu za viganja vyake, alipoikunjua mikono yake,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
13Ndiye aliyeitenga Bahari Nyekundu, ikasimama pande mbili,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
14Akawapitisha Waisiraeli hapo katikati,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
15Ndiye aliyemtosa Farao na vikosi vyake katika Bahari Nyekundu,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
16Ndiye aliyewaongoza nyikani walio ukoo wake,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
17Ndiye aliyepiga wafalme wakuu,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
18Akawaua wafalme wenye nguvu,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
19Kama Sihoni, mfalme wa Waamori,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
20Na Ogi, mfalme wa Basani,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
21Akazitoa nchi zao, zitwaliwe,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
22Zitwaliwe na Waisiraeli walio watumishi wake, ziwe fungu lao,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
23Ndiye aliyetukumbuka, tulipokuwa tumenyenyekezwa,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
24Akatuponya na kutuokoa kwao watusongao,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
25Ndiye anayewapa vilaji wote walio wenye miili,
kwani upole wake ni wa kale na kale.
26Mshukuruni Mungu aliye wa mbingu!
Kwani upole wake ni wa kale na kale.