The chat will start when you send the first message.
1Kwenye mito ya Babeli twalikaa na kulia tulipoikumbuka Sioni,
2katika mifuu iliyoko kule twaliyaangika mazeze yetu.
3Kwani kule waliotuteka walitushurutisha kuimba nyimbo, wao waliotuumiza walitaka, tuwachezee, wakasema: Tuimbieni wimbo wa Sioni!
4Lakini tungaliwezaje kuimba wimbo wa Bwana katika nchi ya ugeni?
5Kama ningekusahau, Yerusalemu, nao mkono wangu wa kuume na usahauliwe![#Yer. 51:50.]
6Ulimi wangu sharti ugandamane na ufizi wangu, nisipokukumbuka, nisipoukweza Yerusalemu kuwa furaha yangu kuu kuliko nyingine zote.
7Bwana, wana wa Edomu na uwakumbukie, walivyoufanyizia Yerusalemu siku ile, waliposema: Bomoeni! Bomoeni mpaka kwenye misingi yake![#Sh. 79:12; Oba. 10-15.]
8Wewe binti Babeli, utakuwa mahame tu. Mwenye shangwe ndiye atakayekulipisha hayo matendo yako, uliyotutendea sisi.
9Mwenye shangwe ndiye atakayewakamata watoto wako wachanga na kuwaponda mwambani.[#Yes. 13:16.]