The chat will start when you send the first message.
1Kwa kuwa mimi nimeendelea pasipo kosa, niamulie, Bwana! Bwana ndiye, nimwegemeaye pasipo kutikisika.
2Nijaribu, Bwana, na kunipima, unichuje mafigo, hata moyo![#Sh. 17:3.]
3Kwani wema wako uko machoni pangu, nami huendelea kukuwia mwelekevu.
4Sikai pamoja na watu walio wapuzi tu, wala walio wenye kinyume siingii mwao.[#Sh. 1:1.]
5Ninachukizwa na mkutano wao wafanyao mabaya, wala sikai pamoja nao wambezao Mungu.
6Nitainawa mikono yangu kwa maji yaondoayo makosa, kisha nitatokea kuzunguka mezani pako, Bwana;[#Sh. 122.]
7ndipo, nitakapozipaza sauti, nikushukuru nikiyasimulia makuu yako yote ya kustaajabu.
8Bwana, napapenda hapo, Nyumba yako ilipo, ndipo mahali, unapokaa utukufu wako.[#Sh. 27:4.]
9Usiikusanye roho yangu pamoja nazo zao wakosaji! Usininyime uzima pamoja nao wauao wenzao!
10Mikononi mwao yamo mapotovu, mikono yao ya kuume imejaa mapenyezo.
11Lakini mimi ninaendelea pasipo kosa; kwa kunihurumia nikomboe!
12Miguu yangu huenda paliponyoka, nimtukuze Bwana katika mikutano.[#Sh. 22:23.]