The chat will start when you send the first message.
1Bwana ni mwanga wangu na wokovu wangu, nimwogope nani? Bwana ni ngome, nilimpoponea, nimstuke nani?[#Sh. 56:5; Yes. 12:2.]
2Wafanyao mabaya wanikaribia, wanile nyama zangu, lakini wanisongao nao wanichukiao watakajikwaa, waanguke.[#Iy. 19:22.]
3Ijapo kikosi kizima kinivizie, moyo wangu hauogopi; vita vikinitokea, ninalo egemeo langu.[#Sh. 3:7.]
4Hili moja, ninalolitaka sana, namwomba Bwana, nikae Nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu, niutazame na kuuchunguza uzuri wake Bwana Jumbani mwake.[#Sh. 23:6; 26:6-8; 42:5; 63:3; 84:4-5.]
5Kwani hunifunika kambini kwake, siku ikiwa mbaya; hunificha fichoni penye hema lake akinikweza mwambani.[#Sh. 31:21; 40:3.]
6Kwa hiyo sasa kichwa changu kitakuwa kimeinuka, kiwashinde wachukivu wangu wanizungukao; napo penye hema lake ndipo, nitakapomtambikia na kumtolea vipaji vya tambiko vya kumshangilia, nimchezee Bwana ngoma na kumwimbia.
7Bwana, isikie sauti yangu, ninapokuita, uniwie mpole na kuniitikia!
8Moyo wangu unakukumbusha neno lako, lile la kwamba: Utafuteni uso wangu! Sasa ninauelekea uso wako, Bwana, kwa kuutafuta.[#5 Mose 4:29.]
9Nawe usiufiche uso wako, usinione! Mtoto wako usimwepuke kwa makali na kumwacha! Wewe ndiwe uliyenisaidia, usinitupe! Mungu aliye wokovu wangu, usiniache!
10Kwani baba na mama wakiniacha, Bwana hunifikiza kwake.[#Yes. 49:15.]
11Bwana, nifundishe njia yako na kuniongoza, nifuate mapito yanyokayo, waninyatiao wasinipate![#Sh. 25:4; 86:11; 139:24.]
12Usinitie mikononi mwao wanisongao! Kwani ndio mashahidi wa uwongo walioniinukia, nao, kusudi wanikorofishe, hunifokea.
13Lakini ninayetegemea ya kwamba: Nitaona meme ya Bwana katika nchi yao walio hai.[#Sh. 142:6; Yes. 38:11.]
14Mngojee Bwana, ujipatie nguvu! Ushupaze moyo wako, umngojee Bwana![#Sh. 31:24.]