The chat will start when you send the first message.
1Mpumbavu husema moyoni mwake: Hakuna Mungu.
2Hawafai kitu, mapotovu yao hutapisha, anayefanya mema hayuko huko.
3Mungu huchungulia toka mbinguni, awatazame wana wa watu, aone, kama yuko mwenye akili anayemtafuta Mungu.[#1 Mose 6:12; Tit. 1:16.]
4Lakini wote pamoja walirudi nyuma, wote ni waovu, hakuna anayefanya mema, hakuna hata mmoja.[#Rom. 3:12.]
5Je? Wale wote wafanyao maovu hawataki kujitambua, wao wanaowala walio ukoo wangu, kama walavyo mkate? Lakini Mungu hawamtambikii!
6Patafika, watakapotetemeka kwa kustuka mastuko yasiyokuwa bado, kwa kuwa Mungu ataitapanya mifupa yao waliokuvizia, kwa kuwa Mungu atakuwa amewatupa, atawatia soni.
7Laiti wokovu wake Isiraeli utokee Sioni, Mungu awarudishe mateka walio wa ukoo wake! Ndipo, Yakobo atakaposhangilia, ndipo, Isiraeli atakapofurahi.[#Luk. 2:25-32.]