The chat will start when you send the first message.
1Kwa mwimbishaji. Fundisho la Dawidi la kuimbia mazeze.
2Sikiliza Mungu, kuomba kwangu!
Usijifiche, nikikulalamikia!
3Niangalie, uniitikie! Ninahangaika kwa kulia kwangu na kupiga kite.
4Kwa sababu adui wananizomea, nao wasiomcha Mungu wananisonga, kwani wanataka, mateso yaniangukie, kwa ukali tu wananipingia.
5Moyo wangu humu ndani yangu unatetemeka, mastuko kama ya kufa yakaniguia;
6masukosuko ya mwili yananijia kwa kuogopa tu, nikapigwa sana na bumbuazi.
7Nikasema: Ningepata mabawa kama ya njiwa, ningeruka na kutua pawapo pote![#Sh. 11:1.]
8Mara wangeniona, nikienda mbali, nikae nyikani.
9Ningepiga mbio kulifikia kimbilio langu, niondoke kwenye upepo uvumao na nguvu kama za kimbunga.
10Waangamize Bwana, ukiwavuruga, wapitane wanaposema, kwani mjini mimeona makorofi na magomvi.[#2 Sam. 17:14.]
11Mchana kutwa na usiku kucha huzungukia kwenye maboma yake, lakini mjini mna mapotovu na maumivu.
12Mle mjini mnaangamika, unyang'anyi na udanganyifu hauondoki katika mitaa yake.
13Tena anayenitukana siye adui yangu, ningevumilia, wala siye mchukivu wangu anayejikuza, aninyenyekeze; kama ndiye, ningejificha, asinione.
14Ila ndiwe wewe mwenzangu, ambaye tuliliana damu, tena ulikuwa mwenyeji wangu mimi.[#Sh. 41:10; 2 Sam. 15:12.]
15Vilikuwa vyenye utamu, jinsi tulivyoendeleana, tulivyokwenda pamoja na makundi ya watu Nyumbani kwake Mungu.
16Kifo na kiwakamate, washuke kuzimuni wakingali wa hai! Kwani katika makao yao na katika mioyo yao yamo mabaya tu.[#4 Mose 16:30-33.]
17Mimi ninamlilia Mungu, yeye Bwana ataniokoa.
18Jioni na mapema na mchana kutwa na nilalamike na kupiga kite; ndipo, atakapoisikia sauti yangu.
19Ataikomboa roho yangu, nikae na kutengemana, wao wasinifikie, ijapo wawe wengi wanaonijia;
20Mungu husikia, naye atawajibu. Yeye ndiye akaaye tangu kale. Wao hawataki kugeuka, kwa kuwa hawamwogopi aliye Mungu.[#Sh. 102:27.]
21Maana wanawakamata nao waliomkalia Mungu, nalo Agano lake wanalipinga.
22Wayasemayo ni mafuta ya midomo, ni matamu kuliko maziwa, lakini mioyoni mwao huwaza vita. Maneno yao, wayasemayo, hulegea kuliko mafuta ya uto, lakini wenyewe ndio panga zilizokwisha kuchomolewa.[#Sh. 57:5; Yer. 9:8.]
23Umtupie bwana yakulemeayo! Yeye atakumalizia, hatamtoa mwongofu, atikisike kale na kale.[#1 Petr. 5:7.]
24Nawe Mungu, uwatelemshe, waje shimoni mwenye kuoza! Wale wenye manza za damu na madanganyo siku zao hawatazifikisha kati, lakini mimi ninakuegemea.[#Sh. 102:25; 2 Fal. 9:33,36-37.]