The chat will start when you send the first message.
1Bwana usinipatilize kwa makali yako, wala kwa machafuko yako yenye moto usinichape![#Sh. 38:2; Yer. 10:24.]
2Bwana, na uniwie mpole, kwani ni mnyonge; kwa kuwa mifupa yangu imestuka, niponye Bwana![#Sh. 51:10.]
3Nayo roho yangu imestuka sana, nawe Bwana, utakawia mpaka lini?[#Sh. 13:2-3.]
4Ee Bwana, rudi, uiopoe roho yangu! Niponye kwa hivyo, ulivyo mwenye utu!
5Kwani kwao waliokwisha kufa hakuna anayekukumbuka, nako kuzimuni yuko nani atakayekushukuru?[#Sh. 30:10; 88:11; 115:17.]
6Kwa kupiga kite nimechoka, nikakiogesha kitanda changu usiku wote, nikayalowesha malalo yangu kwa machozi yangu.
7Macho yangu yamenyauka kwa uchungu, yakachakaa kwa ajili yao wote wanisongao.[#Sh. 31:10; Iy. 17:7.]
8Ondokeni kwangu, nyote mfanyao maovu! Kwani Bwana huzisikia sauti za kilio changu.
9Bwana husikia, ninavyomlalamikia, Bwana huyapokea maombo yangu.
10Adui zangu watapatwa na soni wote kwa kustushwa sana, watarudi nyuma kwa kuingiwa na soni kwa mara moja.[#Sh. 35:4,26; 40:15.]