Mashangilio 61

Kumwombea mfalme.

1Mungu, lisikie lalamiko langu!

2Yaitikie nikuombayo!

3Kwenye mapeo ya nchi ninakuita, moyo wangu ukizimia. Unikweze mwambani! Kwani ni mrefu wa kunishinda.

4Kwani kimbilio langu ndiwe wewe, u mnara wenye nguvu machoni pao adui.[#Sh. 18:2-3; 71:3.]

5Ninataka kuwamo katika kituo chako kale na kale, na kulikimbilia ficho lililomo mabawani mwako.[#Sh. 63:3.]

6Kwani wewe, Mungu, umeyasikia niliyokuapia, ukanigawia fungu lao waliogopao Jina lako.

7Unamwongezea mfalme siku kwa siku, miaka yake iwe ya vizazi na vizazi.[#Sh. 21:5.]

8Akiendelea machoni pake Mungu atakaa kale na kale. Agiza vya upole na vya kweli, vimsimamie![#2 Sam. 7:16.]

9Hivyo nitaliimbia Jina lako kale na kale na kuyalipa siku kwa siku niliyokuapia.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania