The chat will start when you send the first message.
1Mpigieni Mungu shangwe, ninyi nchi zote!
2Uimbieni utukufu wa Jina lake! Mtukuzeni na kumsifu!
3Mwambieni Mungu: Kweli matendo yako ndiyo yanayostaajabisha, kwa nguvu zako nyingi watakunyenyekea nao wachukivu wako.
4Nchi zilizoko zote zinakuangukia, wanakuimbia wewe, nalo Jina lako wanaliimbia.
5Njoni, mvione vioja vya Mungu! Jinsi anavyowaendea wana wa watu, ni vya kustaajabu.
6Bahari aliigeuza kuwa nchi kavu, wakapita kwa miguu kwenye mto mkubwa; kwa hiyo tunamfurahia aliye hivyo.[#2 Mose 14:21; Yos. 3:17.]
7Hutawala kwa uwezo wake mkubwa kale na kale, macho yake huyatazama makabila ya watu, waliomwacha hawatajivuna mbele yake.
8Ninyi makabila ya watu, mtukuzeni Mungu wetu! Pazeni sauti za kumsifu!
9Roho zetu huzipa kuwa zenye uzima, haiachi miguu yetu, ujikwae.
10Kweli ulitujaribu, Mungu, na kutuyeyusha, kama ni fedha, watu wanazoziyeyusha,[#Fano. 17:3.]
11ukatupeleka kifungoni na kututwika mzigo uliotulemea viunoni,
12ukaleta watu, watukanyage vichwa, tukaingia motoni namo majini, lakini ulitutoa mle, ukatukalisha panapo mema mengi.[#Yes. 43:2.]
13Nitakuja, nikupelekee ng'ombe za tambiko Nyumbani mwako, nikulipe hayo, niliyokuapia,
14midomo yangu ilipofumbuka kwa hivyo, nilivyokuwa nimesongeka; ilikuwa hapo, kilipoyasema kinywa changu.
15Nitakupelekea ng'ombe za tambiko zenye mafuta pamoja na nyama za kondoo za vukizo; kweli ni ng'ombe na kondoo, nitakaokutengenezea.
16Njoni, msikilize, nyote mmwogopao Mungu, niwasimulie aliyoifanyizia roho yangu.
17Nilikifumbua kinywa changu, nikamlalamikia, tena ulimi wangu nao ulikuwa umejitega, upate kumtukuza.
18Kama ningalikuwa nimeuelekeza moyo wangu kwenye maovu, Bwana angalikataa kunisikia.[#Fano. 28:9; Yoh. 9:31.]
19Neno hili ni la kweli: Mungu husikia; akaisikiliza nayo sauti ya lalamiko langu.
20Mungu na atukuzwe, maana hakuninyima niliyomwomba, wala hakuninyima upole wake.