The chat will start when you send the first message.
1Wewe Bwana, nimekukimbilia, sitapatwa na soni kale na kale.
2Kwa kuwa u mwongofu, niopoe na kuniponya! Nitegee sikio lako, ukaniokoe!
3Niwie mwamba wenye nguvu, niujie siku zote, maana uliniagia, ya kuwa utaniokoa. Kwani mwamba wangu na boma langu ndiwe wewe.[#Sh. 18:3; 31:3-4.]
4Mungu wangu, niponye mikononi mwao wasiokucha! Namo mikononi mwao wapotovu namo mwao wakorofi!
5Kwani wewe Bwana Mungu, u kingojeo changu, u kimbilio langu tangu hapo, nilipokuwa mtoto.
6Nimejishikiza kwako tangu hapo, nilipozaliwa, wewe ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu; ninakushangilia siku zote.[#Sh. 22:10.]
7Kwao wengi ni kama kielekezo, wakiniona, nawe ndiwe kimbilio langu lenye nguvu.[#Sh. 4:4.]
8Kinywa changu kinazidi kukushangilia, siku zote huutangaza utukufu wako.
9Siku, nitakapokuwa mzee, usinitupe, nguvu yangu itakapoishia, usiniache![#Sh. 71:18.]
10Kwani wachukivu wangu wamekwisha kusema, nao wanaoingoja roho yangu wamekula njama pamoja:
11Mungu amemwacha; mkimbizeni, mmkamate! Kwani hakuna tena atakayemwopoa.
12Wewe Mungu, usiniendee mbali! Mungu wangu, piga mbio, unisaidie!
13Sharti wapatwe na soni, sharti waangamie wao waliotakia mabaya roho yangu. Sharti wajifunike kwa kutwezwa wakiumbuka waliotafuta mabaya ya kunifanyizia.
14Lakini mimi nitangoja siku zote pamoja na kufuliza kukupigia shangwe vivyo hivyo.
15Kinywa changu kitayasimulia mambo ya wongofu wako na kuutangaza wokovu wako siku zote, kwani sijui kuyahesabu, kama ni mangapi.[#Sh. 40:6; 71:8.]
16Ninaendelea bado kwa nguvu za Bwana Mungu zilizo kuu, ninayowakumbusha si mengine, ni wongofu wako tu.
17Mungu, ulinifundisha tangu hapo, nilipokuwa mtoto; kwa hiyo ninayatangaza mataajabu yako.[#1 Sam. 7:12.]
18Sasa napo hapo, nitakapokuwa mzee mwenye mvi, usiniache, Mungu, niwatangazie vizazi vingi kazi za mkono wako nayo matendo yako yenye nguvu kwao wote watakaokuwapo.[#Sh. 71:9; Yes. 46:4.]
19Wongofu wako, Mungu, unakua kufika hata mbinguni, wewe ndiwe ufanyaye mambo makuu. Mungu, afananaye na wewe yuko nani?[#2 Mose 15:11.]
20Wewe ulipotuacha, tuliona masongano mengi na mabaya; lakini utaturudisha tena, utupatie uzima, utatutoa huko ndani ya nchi, utuweke juu yake.[#1 Sam. 2:6.]
21Ukuu, utakaonipa, utazidi, utakaponigeukia, unitulize moyo.
22Nami nitakushukuru na kukupigia pango kwa welekevu wako, Mungu wangu, nitakuimbia na kupiga zeze, wewe Mtakatifu wa Isiraeli.
23Midomo yangu inashangilia, kwa hiyo ninakuimbia, roho yangu inashangilia nayo, kwa maana umeikomboa.
24Nao ulimi wangu unausimulia wongofu wako mchana kutwa, kwani waliotafuta mabaya ya kunifanyizia huiva nyuso kwa soni.