The chat will start when you send the first message.
5Bwana Mungu Mwenye vikosi, utakasirika mpaka lini, ijapo wakulalamikie walio ukoo wako?
6Umewalisha mikate iwalizayo, nayo machozi yao yakawa vinywaji, ulivyowanywesha kwa vikombe.[#Sh. 102:10.]
7Umetuacha, majirani zetu wakapigana wao kwa wao, watupate sisi, nao adui zetu wanatusimanga.
8Mungu Mwenye vikosi, turudishe kwako! Utuangazie uso wako! Ndivyo, tutakavyookoka.[#Sh. 80:4,20.]
9Uko mzabibu, ulioung'oa kule Misri; ukafukuza wamizimu, ukaupanda mahali pao.[#Yes. 5:1-7; Hos. 10:1.]
10Ukaupanulia, uweze kutia mizizi yake, ukaieneza nchi.
11Milima ikafunikwa na kivuli chake, nayo miangati ya Mungu ikafunikwa na matawi yake mengi.
12Ukayaendesha machipukizi yake mpaka baharini, nayo miche yake ukaifikisha kwenye mto mkubwa.
13Mbona umekibomoa kitalu chake, wote wapitao njia wakapata kuuchuma?[#Sh. 89:42.]
14Nguruwe wa mwituni wakauchimbachimba, nao nyama wa porini wakaula.
15Mungu Mwenye vikosi, tunakuomba: Rudi! Chungulia toka mbinguni, uvione! Huo mzabibu wako uutazama!
16Uuangalie! Maana mkono wako wa kuume ndio ulioupanda, ni mwanao, uliyemkuza na kumpa nguvu.
17Umechomwa na moto, ukakatwakatwa; lakini kwa makaripio ya uso wako wataangamia.
18Mtu, mkono wako wa kuume uliyemweka, mkono wako na umshike! Na umshike huyo mwana wa mtu, uliyemkuza na kumpa nguvu!
19Nasi hatutaki kuondoka kwako wewe; kusudi tupate kulikuza Jina lako, tupe uzima tena!
20Bwana Mungu Mwenye vikosi, turudishe kwako! Utuangazie uso wako! Ndivyo, tutakavyookoka.[#Sh. 80:4,8.]