The chat will start when you send the first message.
1Ulijengwa na kushikizwa kwenye milima iliyo mitakatifu.
2Bwana huipenda milango wa Sioni kuliko makao yote ya Yakobo.
3Mambo yenye utukufu hutangazwa mwako ulio mji wa Mungu.
4Nitakumbusha Rahabu na Badeli miongoni mwao wanijuao, waliozaliwa mumo humo watazameni: wamo Wafilisti na Watiro, hata Wanubi![#Yes. 30:7; Sh. 68:32; 89:11.]
5Sioni hutukuzwa kwamba: Watu wa makabila yote huzaliwa mle! Naye Alioko huko juu ndiye anayeushupaza.
6Bwana akiyahesabu makabila ya watu ataandika kwamba: Fulani na fulani walizaliwa mlemle.
7Nao wenyewe watacheza ngoma pamoja na kuimba: Visima vyangu vyote vimo mwako!