The chat will start when you send the first message.
1Bwana uliye Mungu mwenye lipizi, Mungu uliye mwenye lipizi, tokea![#5 Mose 32:35.]
2Wewe uliyeiamulia nchi, inuka! Warudishie wenye majivuno matendo yao![#1 Mose 18:25.]
3Wasiokucha, Bwana, wakubeze mpaka lini? Hao wasiokucha waseme makuu yao mpaka lini?
4Wanazidi kusimuliana na kusema makorofi, wote wafanyao maovu hujisemea hivyo.
5Walio ukoo wako huwaponda, walio fungu lako huwatesa;
6wajane na wageni huwanyonga, wafiwao na wazazi huwaua.
7Bwana havitazami! Ndivyo, wanavyosema, Mungu wa Yakobo havitambui![#Sh. 10:11.]
8Vitambueni, ninyi msiojua kitu, mlio wa ukoo wetu! Nanyi wajinga, mtaerevuka lini?[#Sh. 92:7.]
9Aliyelifanya sikio, asisikie? Aliyeliumba jicho, asione?[#2 Mose 4:11.]
10Achapuaye wamizimu, asipatilize? Siye yeye afundishaye watu, wapate kujua?
11Lakini Bwana huyatambua mawazo ya watu, ya kuwa hayo ndiyo yaliyo ya bure.[#1 Kor. 3:20.]
12Mwenye shangwe ni mtu, umchapuaye, wewe Bwana, na kumfundisha yaliyomo katika Maonyo yako, ayajue.[#Sh. 19:12-14; Iy. 5:17.]
13Hivyo atajituliza kwa kuona, siku za wabaya zilivyo, mpaka wasiokucha wachimbiwe mashimo.[#Sh. 37:7.]
14Kwani Bwana hatawatupa walio ukoo wake, nao walio fungu lake hatawaacha.[#Rom. 11:1-2.]
15Kwani pako bado, watu wanapoamuliwa kwa wongofu wote wenye mioyo inyokayo watapafuata hapohapo.
16Yuko nani atakayeinuka kuwa upande wangu, nikipigana nao wabaya? Yuko nani atakayesimama kwangu, nikipigana nao wafanyao maovu?
17Kama Bwana asingekuwa anisaidiaye, roho yangu ingekuwa imekwisha kulala mahali palipo kimya.[#Sh. 115:17.]
18Niliposema moyoni: Mguu wangu umejikwaa, ndipo, upole wako, Bwana, uliponishikiza.
19Mawazo yalipozidi kuwa mengi moyoni mwangu, ndipo, matulizo yako yalipoichangamsha roho yangu.[#2 Kor. 1:4-5.]
20Je? Wewe uko na bia napo panapoamuliwa kwa ukorofi? Maana ndipo panapoleta maumivu kwa kuyapotoa yaliyo ya kweli.
21Wao huishambulia roho yake aliye mwongofu, humwaga damu zao wasiokosa.
22Lakini Bwana ndiye atakayekuwa ngome yangu, yeye Mungu ni mwamba wangu wa kuukimbilia.
23Atawalipiza mapotovu yao na kuwamaliza kwa ubaya wao, Bwana Mungu wetu atawamaliza kweli.