The chat will start when you send the first message.
1Huu ndio ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu, awaonyeshe watumwa wake mambo yatakayo kufanyika upesi. Ndipo, alipomtuma malaika wake, amweleze mtumwa wake Yohana, hayo mambo.[#Ufu. 1:19.]
2Yeye ndiye aliyelishuhudia Neno la Mungu, hata ushuhuda wa Yesu Kristo, maana aliyaona yote.[#Ufu. 1:9; 6:9.]
3Wenye shangwe ndio wanaoyasoma nao wanaoyasikia maneno ya ufumbuo huu na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwani siku ziko karibu.[#Ufu. 22:7,10; Kol. 4:16.]
4Mimi Yohana nawasalimu ninyi makundi saba ya wateule yaliyoko Asia. Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwake yeye aliopo, aliyekuwapo, atakayekuja! Tena unatoka nako kwao roho saba walioko mbele ya kiti chake cha kifalme,[#Ufu. 1:8; 3:1; 5:6; 2 Mose 3:14-15.]
5nako kwa Yesu Kristo; huyu ni shahidi mwelekevu na mzaliwa wa kwanza wa wafu na mkuu wa wafalme wa nchini. Yeye alitupenda, akatukomboa katika makosa yetu kwa damu yake,[#Ufu. 3:14; 19:16; 1:18; 7:14; Yoh. 18:37; Kol. 1:18; Ebr. 9:14.]
6akatupatia ufalme, tuwe watambikaji wa Baba yake Mungu. Wake yeye ni utukufu na uwezo kale na kale pasio mwisho. Amin.[#Ufu. 5:10; 2 Mose 19:6; Yes. 61:6; Mat. 24:30; Yoh. 19:34; 1 Petr. 2:5,9.]
7Tazameni, anakuja mawinguni, macho yote yatamwona, nayo yao waliomchoma; ndipo, makabila yote ya nchini yatakapomlilia. Ndio, ni kweli.[#Dan. 7:13; Zak. 12:10; Yoh. 19:37.]
8Mimi ni A na O, ni kwamba: Mwanzo na Mwisho;
ndivyo, Bwana Mungu anavyosema
aliopo, aliyekuwapo, atakayekuja, aliye Mwenyezi.
9Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenzenu wa maumivu na wa ufalme na wa uvumilivu, tupewao na Yesu, nilikuwa katika kisiwa kinachoitwa Patimo. Nilikuwako, maana nalilitangaza Neno la Mungu na kumshuhudia Yesu.
10Nikawapo kiroho penye siku ya Bwana, nikasikia nyuma yangu sauti kuu kama ya baragumu,[#Ufu. 1:15.]
11kwamba: Mimi ni A na O, wa kwanza na wa mwisho; unayoyaona, yaandike katika kitabu, ukitume kwa yale makundi saba ya wateule yaliyoko Efeso na Simirna na Pergamo na Tiatira na Sarde na Filadelfia na Laodikia![#Ufu. 1:8,17; 2:8; 22:13.]
12Nikapinduka, nione, kama ni sauti ya nani iliyosema nami. Nami nilipopinduka nikaona taa saba za dhahabu.[#Ufu. 1:20.]
13Katikati ya hizo taa nikaona mwenye kufanana na Mwana wa mtu. Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu, napo kifuani alikuwa amejifunga mkanda wa dhahabu.[#Ufu. 2:1; Dan. 7:13; 10:5.]
14Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama pamba au kama theluji, macho yake yalikuwa kama moto unaowaka.[#Ufu. 2:18; 19:12; Dan. 7:9-10,14; 10:6.]
15Miguu yake ilifanana na shaba nyekundu imulikayo motoni mwa jikoni, sauti yake ilikuwa kama uvumi wa maji mengi.[#Ufu. 2:18.]
16Namo mkononi mwake mwa kuume alishika nyota saba, namo kinywani mwake mlitoka upanga mkali ulio na makali pande mbili. Nao uso wake ulikuwa kama jua, liking'aa kwa nguvu zake.[#Ufu. 1:20; 2:1; 2:12,16; 19:15.]
17Nami nilipomwona nikaanguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Ndipo, aliponibandikia mkono wake wa kuume, akasema: Usiogope! Mimi ndiye wa kwanza na wa mwisho[#Dan. 8:18; 10:15-19.]
18na mwenye uzima. Nalikuwa nimekufa, tena tazama, mimi niko, ni mwenye uzima kale na kale pasipo mwisho. Ninazo funguo za kifo na za kuzimu.
19Basi, yaandike mambo, uliyoyaona, nayo yaliyopo nayo yatakayokuwapo, haya yatakapokwisha!
20Liandike fumbo la zile nyota saba, ulizoziona mkononi mwangu mwa kuume, nalo fumbo la zile taa saba za dhahabu. Zile nyota saba ndio malaika wa makundi saba ya wateule, nazo taa saba ndio makundi saba ya wateule.[#Mal. 2:7.]