The chat will start when you send the first message.
1Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwani mbingu za kwanza nazo nchi za kwanza zilikuwa zimetoweka, nayo bahari ilikuwa haiko tena.[#Ufu. 20:11; Yes. 65:17; 2 Petr. 3:13.]
2Nikauona mji mtakatifu wa Yerusalemu mpya, ukishuka toka mbinguni kwake Mungu. Ulikuwa umetengenezwa kama mchumba mke aliyepambiwa mumewe.[#Ufu. 19:7-8; Gal. 4:26; Ebr. 11:10,16; 12:22.]
3Nikasikia sauti kuu iliyotoka kitini mwa kifalme, ikisema: Tazama, kituo chake Mungu cha kukaa pamoja na watu! Humo atatua pamoja nao, nao watakuwa watu wake, naye Mungu atakuwa pamoja nao,[#Ez. 37:27; 48:35.]
4atayafuta machoni mwao machozi yote, hata kufa hakutakuwapo tena, wala sikitiko, wala kilio, wala maumivu hayatakuwa tena. Kwani mambo ya kwanza yatakuwa yamekwisha pita.[#Ufu. 7:17; Yes. 25:8; 35:10.]
5Kisha yule aliyekaa kitini mwa kifalme akasema: Tazama, navifanya vyote kuwa vipya. Akasema: Andika! Kwani maneno haya yapasa kutegemewa, maana ni ya kweli.[#Ufu. 4:2; 5:1; 2 Kor. 5:17.]
6Akaniambia: Yamekwisha kufanyika. Mimi ni A na O, ni kwamba: Mwanzo na mwisho. Aonaye kiu, mimi nitampa bure ya kunywa toka kisimani mwenye maji ya uzima.[#Ufu. 1:8; 22:17.]
7Mwenye kushinda atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwana wangu.[#Ufu. 2:7; Zak. 8:8.]
8Lakini walio waoga nao wakataao kunitegemea nao wachukizao kwa ubaya wao nao walio wauaji na wagoni na wachawi na watambikia vinyago na waongo wote fungu lao hao limo katika ziwa linalowaka moto wa viberitiberiti. Huko ndiko kufa kwa pili.[#Ufu. 20:14; 22:15; Ebr. 10:38-39.]
9Pakaja mmoja wao wale malaika saba wenye vile vyano saba vilivyojaa mapigo saba ya mwisho, akasema nami akaniambia: Njoo! Nitakuonyesha mchumba aliye mkewe Mwana kondoo.[#Ufu. 15:1,6-7; 19:7.]
10Akanichukua kiroho, akanipeleka juu ya mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu wa Yerusalemu ushukao toka mbinguni kwake Mungu.[#Ez. 40:2.]
11Utukufu wake ni ule wa Mungu; mwanga uuangazao umefanana nao wake kile kito kivipitacho vito vyenziwe vyote, kilicho kama kijiwe cha yaspi kimulikacho.[#Ufu. 21:3,23; Yes. 60:1-2.]
12Ulikuwa na boma ya mawe kubwa na refu, lililokuwa na malango kumi na mawili, napo malangoni juu palikuwa na malaika kumi na wawili. Hata majina yalikuwa yameandikwa humo malangoni, ndiyo yale ya mashina kumi na mawili ya wana wa Isiraeli.[#Ez. 48:31-35.]
13Maawioni kwa jua kulikuwa na malango matatu, nako kaskazini malango matatu, nako kusini malango matatu, nako machweoni kwa jua malango matatu.
14Hilo boma la mji lilikuwa lenye misingi kumi na miwili, namo misingini mlikuwamo majina kumi na mawili, ni ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana kondoo.
15Yule aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu wa kupimia, apate kuupima mji na malango yake na boma lake.[#Ez. 40:3.]
16Huo mji ulikuwa umejengwa kwenye pembe nne, urefu wake ni sawa na upana wake; akaupima mji kwa ule mwanzi, ukawa kama mwendo wa siku za mchana mia nne. Urefu wake na upana wake nao urefu wake wa juu ni sawa.[#Ez. 48:16-17.]
17Akalipima boma lake, likawa la mikono 144 kwa kipimo cha mtu kilichokuwa cha malaika naye.
18Hili boma lake lilikuwa limejengwa na mawe ya yaspi, nao mji ulikuwa wa dhahabu ionayo, kama kioo kinavyoona.
19Misingi ya boma la mji ilikuwa imepambwa na vito vyote: msingi wa kwanza ulikuwa wa yaspi, wa pili wa safiro, wa tatu wa kalkedoni, wa nne wa sumaradi,[#Yes. 54:11-12.]
20wa tano wa sardoniki, wa sita wa sardio, wa saba wa krisolito, wa nane wa berilo, wa tisa wa topazio, wa kumi wa krisopuraso, wa kumi na moja wa yakuti, wa kumi na mbili wa ametisto.
21Malango yake kumi na mawili yalikuwa lulu kumi na mbili, kila lango moja lilikuwa limetengenezwa kwa lulu moja. Hata uwanja mkuu wa mji ulikuwa wa dhahabu uonao, kama kioo kiangafu.[#Ufu. 22:2.]
22Jumba la kuombea sikuliona humo mwake, kwani Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana kondoo ni ombeo lao,
23Tena mji hautumii jua wala mwezi, upate kuwa wenye mwanga. Kwani utukufu wa Mungu huuangaza, naye Mwana kondoo ni taa yake.[#Ufu. 22:5; Yes. 24:23; 60:19-20.]
24Nao wamizimu wataujia huo mwanga wake, nao wafalme wa nchi huuingiza utukufu wao mumo humo.[#Yes. 60:3,5.]
25Hayo malango yake hayafungwi kamwe mchana, maana usiku haumo[#Ufu. 22:5; Yes. 60:11; Zak. 14:7.]
26Hata utukufu na urembo wa wamizimu wataungiza mwake.
27Lakini kilicho kibaya cho chote hakitaingia kamwe mwake, wala mwenye kufanya machukizo na uwongo, ila wale tu walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo.[#Ufu. 20:15; Fil. 4:3.]