The chat will start when you send the first message.
1Basi, niseme: Mungu aliwatupa walio ukoo wake? La, sivyo! Kwani hata mimi ni Mwisiraeli, ni wa uzao wake Aburahamu, ni wa shina la Benyamini.[#Sh. 94:14; Yer. 31:37; Fil. 3:5.]
2Mungu hakuwatupa walio ukoo wake,
aliowatambua kale. Au hamyajui, Maandiko yanayoyasema, Elia alipomlalamikia Mungu kwa ajili ya Waisiraeli?
3Akasema:
Bwana, wafumbuaji wako wamewaua,
wakapabomoa pote pa kukutambikia,
nikasalia mimi peke yangu,
tena roho yangu nayo wanaitafuta, waichukue.
4Lakini jibu la Mungu linamwambia nini?
Nimejisazia watu 7000 wasiompigia Baali magoti.
5Basi, vivyo hata siku hizi za sasa liko sazo lililochaguliwa kupata magawio.[#Rom. 9:27.]
6Lakini yakiwa magawio, siyo malipo ya matendo. Kama sivyo, magawio hayangekuwa magawio, kwani kama huko ni kulipa matendo, siko kugawia; kama sivyo, matendo yangekuwa ya bure.
7Basi inakuwaje? Waisiraeli waliyoyatafuta, hawakuyafikia, lakini wachaguliwao tu ndio walioyafikia. Lakini wale wengine walishupazwa mioyoni mwao, kama ilivyoandikwa:[#Rom. 9:31.]
8Mungu aliwapa roho ya usingizi
na macho yasiyoona na masikio yasiyosikia
mpaka siku hii ya leo.
9Naye Dawidi anasema:
Sharti meza zao ziwawie matanzi na mitego,
wanaswe, walipizwe mabaya yao.
10Macho yao na yatiwe giza, wasione,
migongo yao nayo ipindike siku zao zote!
11Basi, niseme: Walijikwalia, waanguke tu? La, sivyo! Ila maanguko yao yamewaletea wamizimu wokovu, wenyewe wawaonee wivu, wapate kujikaza.[#Rom. 10:19; Tume. 13:46.]
12Lakini maanguko yao yakiwa yameuletea ulimwengu mapato mengi, nako kushindwa kwao kukiwa kumewaletea wamizimu mapato mengi, je? Hapo, watakapokuja wote, hayo mapato hayataongezeka sanasana?
13Nasema nanyi mlio wamizimu. Mimi kwa hivyo, nilivyo mtume wa wamizimu, na niutukuze utumishi wangu!
14Hivyo labda nitawatia wivu walio ndugu zangu kimtu, nipate kuwaokoa mmojammoja.[#1 Kor. 9:22; 1 Tim. 4:16.]
15Kwani hapo walipotupwa waliwapatia wao wa ulimwengu wokovu; basi, hapo watakapopokelewa watawapatia nini, isipokuwa kufufuka na kutoka penye wafu?
16Tena limbuko likiwa linatakata, limbiko nalo litatakata. Tena shina likiwa limetakata, matawi nayo yatatakata.[#4 Mose 15:20.]
17Lakini kama yako matawi yaliyovunjwa na kuondolewa, kisha wewe uliye mdanzi tu ukatiwa mahali pao, ukagawiwa fungu lako la shina na utomvu wa ule mchungwa,[#Ef. 2:11-14,19.]
18usijivune kwao yale matawi! Lakini ukijivuna ujue: si wewe unaolipa shina nguvu, ila shina linakupa nguvu wewe![#Yoh. 4:22.]
19Labda utasema: Matawi yalivunjiwa mimi, nipate pa kutiwa.
20Ni vizuri; yalivunjika mle, kwa ajili hayakushikamana; wewe nawe ukashinda mle kwa nguvu ya kushikamana. Usijikweze, ila uogope!
21Kwani Mungu kama asivyoyaonea uchungu yale matawi yaliyochipukia mlemle, hata wewe hatakuonea uchungu.
22Basi, humo utazame utu na ukali wake Mungu! Ukali uko kwao walioanguka, lakini kwako wewe uko utu wake Mungu, ukifuliza kuukalia huo utu. Ikiwa sivyo, hata wewe utakatwa.[#Yoh. 15:2,4; Ebr. 3:14.]
23Nao wale watatiwa tena, wasipofuliza kuukalia ukatavu; maana Mungu yuko na nguvu ya kuwatia mle tena.[#2 Kor. 3:16.]
24Tazama: Wewe ulichipuka katika mdanzi, kisha ukakatwa humo, ukatiwa katika mchungwa usio shina lako; basi, wale waliochipukia mlemle, ni vigumu gani kuwatia tena katika mchungwa wao wenyewe?
25Kwani sitaki, ndugu, mkose kulijua fumbo hili, mkajiwazia wenyewe kuwa wenye akili. Waisiraeli wengine wao wameshupazwa mioyoni, mpaka wingi wa wamizimu utakapokwisha kuingia.[#Luk. 21:24; Yoh. 10:16; 2 Kor. 3:14-16.]
26Hivyo ndivyo, Waisiraeli wote watakavyookoka, kama ilivyoandikwa:
Mle Sioni atatokea mponya;
ndiye atakayemgeuza Yakobo, aache mabezo.
27Nalo hili ni agano, ninalolifanya nao:
Nitayaondoa makosa yao.
28Kwa hivyo, wanavyoukataa Utume mwema, ndio wachukivu kwa ajili yenu; lakini kwa hivyo, walivyochaguliwa, ndio wapendwa kwa ajili ya baba zao.
29Kwani Mungu hayajutii magawio na wito wake.
30Kama ninyi: Kale mlimkataa Mungu, lakini sasa mmehurumiwa kwa ajili ya ukatavu wao hao;
31vivyo hivyo hata hao sasa wameikataa ile huruma iliyowatokea, kwamba nao siku ziwafikie, watakapohurumiwa.
32Kwani Mungu aliwaunga wote pia, wamkatae, apate kuwahurumia wote.[#Gal. 3:22; 1 Tim. 2:4.]
33*Tazameni, jinsi ujuzi na utambuzi wake Mungu unavyofurika kuwa mwingi! Kweli maamuzi yake hayachunguziki, njia zake nazo hazinyatiliki![#Rom. 9:23; 10:12; Yes. 45:15; 55:8-9.]
34Kwani yuko nani aliyeyatambua mawazo ya Bwana? Au yuko nani aliyekula njama naye?[#Iy. 15:8; Yes. 40:13; Yer. 23:18; 1 Kor. 2:16.]
35Au yuko nani aliyeanza kumpa kitu, apate kulipwa naye?[#Iy. 41:3-11.]
36Kwani yote yalitoka kwake yeye, yakafanywa naye yeye, tena yatarudi kwake yeye. Yeye ndiye atakayetukuzwa kale na kale. Amin.*