Waroma 12

Waroma 12

Kumtumikia Mungu kwa Kweli.

1*Nawaonya, ndugu, kwa hivyo, Mungu alivyowaonea uchungu, mtoe miili yenu, iwe vipaji vitakatifu vya tambiko vyenye uzima vya kumpendeza Mungu; huko ndiko kumtumikia Mungu kunakoelekea.[#Rom. 6:13; Yoh. 4:24; 1 Petr. 2:5.]

2Msijifananishe nao walio wa siku hizi tu, ila mgeuke, mpewe mawazo mapya, mpate kuyapambanua, Mungu ayatakayo kwamba: Ni mema ya kumpendeza hapo, yatakapotimilika.[#Ef. 4:23; 5:10,17.]

3Kwa kipaji, nilichogawiwa, namwambia kila mmoja wa kwenu, asiwaze makuu yanayopapita hapo panapopasa kuwaza. Ila awaze, jinsi atakavyopata kuerevuka, kila mtu, kama Mungu alivyomgawia kumtegemea.[#Mat. 20:26; 1 Kor. 12:11; Ef. 4:7.]

4Kwani ni vivyo hivy: tunavyo viungo vingi katika mwili mmoja, lakini viungo vyote havina kazi moja.[#1 Kor. 12:12.]

5Vivyo sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa maana tu wa Kristo, tena kila mmoja na mwenzake tu viungo tu.[#1 Kor. 12:27; Ef. 4:25.]

6Tena vipaji, tulivyopewa ni vingi, kila mtu anacho chake, kama alivyogawiwa.*[#1 Kor. 12:4.]

*Mwenye ufumbuaji sharti aupatanishe na kumtegemea Mungu.

7Mwenye utumishi sharti atumike kweli! Mfunzi na aushike ufundisho wake![#1 Petr. 4:10-11.]

8Mwenye kuonya sharti aonyeke! Mwenye kugawia sharti anyenyekee! Aliye mkuu sharti ajihimize! Mwenye kutunza wengine sharti avifurahie![#Mat. 6:3; Luk. 14:12; 2 Kor. 8:2; 9:7.]

9Mapendano yasiwe ya uwongo! Yachukieni yaliyo mabaya mkigandamiana nayo yaliyo mema![#Amo. 5:15; 1 Tim. 1:5.]

10Mpendane kindugu kwa mioyo, tena mwongozane na kuheshimiana ninyi kwa ninyi![#Yoh. 13:4-15; Fil. 2:3; 2 Petr. 1:7.]

11Msilegee, panapotakwa wenye kujikaza! Roho zenu ziwe zenye moto mnapomtumikia Bwana![#Ufu. 3:15.]

12Furahini, ya kwamba mnacho kingojeo! Yavumilieni maumivu! Fulizeni kuomba![#1 Tes. 5:17.]

13Changeni bia, mwapatie watakatifu, wanavyovikosa! Wageni wapokeeni pasipo kunung'unika![#Ebr. 13:2; 3 Yoh. 5-8.]

14Changeni bia, mwapatie watakatifu, wanavyovikosa! Wageni wapokeeni pasipo kunung'unika![#Mat. 5:44; Tume. 7:59; 1 Kor. 4:12.]

15Furahini pamoja nao wafurahio! Lieni pamoja nao waliao![#Sh. 35:13.]

16Mioyo yenu nyote sharti iwe mmoja! Msiyatunukie yaliyo makuu, ila yaliyo manyonge, mfuatane nayo! Msijiwazie wenyewe kuwa wenye akili!*[#Rom. 15:5; Fano. 3:7.]

Lipizi linalofaa.

17*Msimlipe mtu maovu kwa maovu! Yawazeni yaliyo mazuri mbele ya watu wote![#Yes. 5:21; 1 Tes. 5:15.]

18Kwa hivyo, mlivyo, mwe wenye kupatana na watu wote, ikiwezekana![#Mar. 9:50; Ebr. 12:14.]

19Wapendwa, msijilipize wenyewe, ila jitengeni, makali (ya Mungu) yapate kutokea! Kwani imeandikwa: Bwana anasema:

Lipizi ni langu mimi, ni mimi nitakayelipisha.

20Lakini mchukivu wako akiwa ana njaa, mpe chakula!

Akiwa ana kiu, mpe cha kunywa!

Kwani ukivifanya hivyo,

utampalia makaa ya moto kichwani pake.

21Usishindwe nayo yaliyo maovu, ila maovu uyashinde kwa mema!*

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania