The chat will start when you send the first message.
1*Kila mtu na autii ukuu! Maana uko na nguvu kumpita yeye. Kwani hakuna ukuu usiotoka kwa Mungu; nao wote ulioko umewekwa na Mungu.[#Fano. 8:15; Yoh. 19:11; Tit. 3:1; 1 Petr. 2:13,17.]
2Kwa hiyo mwenye kuubisha ukuu hulibisha tengenezo lake Mungu. Lakini wabishi watajipatia hukumu.
3Kwani wenye nguvu hawaogopeshi, ukifanya mema, ila ukifanya maovu. Nawe usipotaka kuuogopa ukuu, fanya yaliyo mema! Hivyo utapata kusifiwa nao.[#1 Petr. 2:13-14.]
4Kwani ukuu humtumikia Mungu, ukupatie mema. Lakini unapofanya maovu ogopa! maana haushiki upanga bure tu. Kwani humtumikia Mungu, humlipiza kwa ukali kila afanyaye kiovu.[#Sh. 82:6.]
5Kwa hiyo inatupasa kutii, si kwa ajili ya ukali tu, ila hata kwa ajili ya mioyo, itung'ae.
6Kwa hiyo mnatoa hata kodi, kwani wao ni watumishi wa Mungu wanaoifuliza kazi hiihii tu.
7Basi, walipeni wote yawapasayo: Mtoza kodi mpeni kodi yake! Mwenye kuchanga mpeni chango lake! Mwenye kuogopesha mwogopeni! Mwenye kuheshimiwa mheshimuni![#Mat. 22:21.]
8Msiwe wadeni wa mtu ye yote, isipokuwa wa kupendana! Kwani anayempenda mwenziwe ameyatimiza Maonyo.[#Gal. 5:14; 1 Tim. 1:5.]
9Kwani kule kwamba:
Usizini! Usiue! Usiibe! Usishuhudie uwongo! Usitamani!
na kama liko agizo jingine, yanaunganika yote katika neno hili:
Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe!
10Ukimpenda mwenzio huwezi kumfanyia kiovu. Kwa hiyo kupendana ndiko kuyatimiza Maonyo.*[#1 Kor. 13:4; Mat. 22:40.]
11*Fanyeni hivyo mkizijua siku hizi, kwamba saa imekwisha fika ya kuamka katika usingizi! Maana wokovu wetu sasa uko karibu kuliko siku zile, tulipoanza kumtegemea Bwana.[#Ef. 5:14; 1 Tes. 5:6-7.]
12Usiku umefikia kucha, mchana upambazuke: kwa hiyo tuziache kazi za giza, tujivike mata ya mwanga![#Ef. 5:11; 1 Yoh. 2:8.]
13Tushike mwenendo upasao mchana! Tusiwe walafi na walevi, wala wagoni na waasherati, wala wagomvi na wenye wivu![#Luk. 21:34; Ef. 5:18.]
14Ila jivikeni Bwana Yesu Kristo! Itunzeni miili yenu na kuiangalia, isishindwe na tamaa!*[#1 Kor. 9:27; Gal. 3:27.]