Waroma 15

Waroma 15

Mapatano ya Kikristo.

1Sisi tulio wenye nguvu imetupasa kuyavumilia manyonge yao wenye kukosa nguvu, tusijipendeze wenyewe.[#Rom. 14:1.]

2Kwetu kila mmoja sharti ampendeze mwenziwe, tusaidiane kujengana vizuri![#1 Kor. 9:19; 10:23-24,33.]

3Kwani naye Kristo hakujipendeza mwenyewe; ila ilikuwa, kama ilivyoandikwa:

Masimango yao wanaokusimanga yameniguia mimi.

4*Kwani yote yaliyoandikwa kale yamendikwa, yatufundishe, tupate kukishika kingojeo chetu tukivumilia, tena tukitulizwa mioyo na yale Maandiko.[#Rom. 4:23-24; 1 Kor. 10:11.]

5Naye Mungu mwenye uvumilivu na mwenye kuituliza mioyo ya watu awape, mioyo yenu nyote iwe mmoja tu, kama inavyowapasa walio wa Kristo Yesu![#Fil. 3:16.]

6Hivyo mtamtukuza Mungu, Baba ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja.

7Kwa hiyo mpokeane, kama Kristo alivyotupokea na sisi, Mungu atukuzwe!

8Kwani nasema: Kristo aliwatumikia waliotahiriwa, ajulishe, ya kuwa Mungu ni mkweli, navyo viagio, baba walivyopewa, akavipatia nguvu.[#Mat. 15:24; Tume. 3:25.]

9Tena anasema: Wamizimu humtukuza Mungu kwa ajili ya kuhurumiwa, kama ilivyoandikwa:

Kwa hiyo nitakuungama kwenye wamizimu,

nalo Jina lako na niliimbie.

10Tena anasema:

Furahini, enye wamizimu, pamoja nao walio ukoo wake!

11Na tena:

Mshangilieni Bwana, ninyi wamizimu wote,

makabila yote ya watu yamsifu!

12Tena Yesaya anasema:

Shinani mwa Isai ataondokea mwenye kuwatawala wamizimu;

huyo ndiye, wamizimu watakayemngojea.

13Naye Mungu, mnayemngojea, awajaze ninyi nyote furaha na utengemano kwa hivyo, mnavyomtegemea, kingojeo chenu kiongezwe nguvu itokayo kwa Roho Mtakatifu!*

Pato la utume wa Paulo.

14Nami mwenyewe, ndugu zangu, nayashika moyoni, kama yalivyo kweli, ya kuwa mema yenu ninyi ni mengi, tena utambuzi wenu ni mwingi, mkaweza hata kuonyana wenyewe.

15Kwa hiyo nimejipa moyo wa kuwaandikia neno mojamoja na kutokeza maana kama mtu anayewakumbusha. Kwani hiki ndicho kipaji changu, nilichogawiwa na Mungu,[#Rom. 1:5; 12:3.]

16nimtumikie Kristo Yesu nikiwatangazia wamizimu Utume mtakatifu wa Mungu na kuwaombea, kusudi wawe kipaji cha tambiko kipendezekacho, kwa kuwa kimetakaswa katika Roho Mtakatifu.[#Rom. 11:13; Fil. 2:17.]

17Basi, kwa hivyo, ninavyoshikamana na Kristo Yesu, ninaweza kujivunia kazi zake Mungu.

18Kwani sitajipa moyo wa kusema neno au tendo lo lote, asilolitenda Kristo hapo, nilipoleta wamizimu, wapate kumtii;[#Rom. 1:5; 2 Kor. 3:5.]

19kwani nguvu iliyowashinda ilikuwa ya vielekezo na ya vioja vyake, tena ile ya Roho takatifu. Hivyo nimeutangaza Utume mwema wa Kristo po pote, nikaanza Yerusalemu, nikaifikisha hata Iliriko na kuzieneza nchi zote zilizoko pembenipembeni.[#Mar. 16:17; Tume. 19:11-12.]

20Nikajitunukia, nisiipige hiyo mbiu njema mahali, Kristo alipokwisha kutangazwa, maana nisiujengee msingi wa mtu mwingine,[#2 Kor. 10:15-16.]

21ila yawe, kama yalivyoandikwa:

Watakaomwona ndio wasioambiwa Neno lake

nao wasiolisikia watalijua maana.

Anataka kufika Roma.

22Kwa ajili hiyo nalizuiliwa mara nyingi kuja kwenu.[#Rom. 1:13.]

23Lakini sasa katika nchi za upande huu hakuna, nilikosaza, tena tangu miaka mingi ninatunukia, nije kwenu;[#Rom. 1:10-11.]

24nitawafikia hapo, nitakapokwenda Spania. Kwani natazamia kuonana nanyi, nitakapopita, nisindikizwe nanyi kwenda huko; lakini kwanza tupeane kikomo cha maneno na kufurahishana kitambo.[#1 Kor. 16:6.]

25Lakini sasa ninakwenda Yerusalemu, niwatumikie watakatifu.[#Tume. 18:21; 19:21; 20:22.]

26Kwani Wamakedonia na Waakea wamependezwa kuchanga machango ya kuwasaidia watakatifu walio maskini huko Yerusalemu.[#1 Kor. 16:1; 2 Kor. 8:1-4; 9:2,12.]

27Nao walichanga kwa kupendezwa, tena ndio wadeni wao. Maana wamizimu wakigawiwa nao mali za Kiroho, imewapasa nao kuwatumikia hao na kuwagawia mali za kimtu.[#Rom. 9:4; 1 Kor. 9:11.]

28Basi, nitakapolimaliza jambo hilo, nikiwapa pato hilo na kulishuhudia, nitaondoka kwenda Spania na kupitia kwenu.

29Nami najua, ya kuwa nitakapokuja kwenu nitakuja mwenye mema yote, Kristo anayotupa.[#Rom. 1:11.]

30Lakini ndugu, nawahimiza kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo na kwa hivyo, tunavyopendana Rohoni, mnipiganie na kuniombea kwa Mungu,[#2 Kor. 1:11; Fil. 1:27; 2 Tes. 3:1.]

31nipate kupona katika wale wasiotii huko Yudea, tena huu utumishi wangu upendezeke kwao watakatifu huko Yerusalemu,

32nami nipate kuja kwenu na kufurahi, tupatiane vituo, Mungu akitaka.

33Naye Mungu mwenye utengemano awe pamoja nanyi nyote! Amin.[#Rom. 16:20.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania