The chat will start when you send the first message.
1Nawaagiziani ndugu yetu Febe aliye mtumishi mke wa wateule wa Kenkerea,
2mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu, tena mmsaidie jambo lo lote, atakalopaswa nanyi. Kwani mwenyewe alitunza wengi, hata mimi.
3Nisalimieni Puriska na Akila waliofanya kazi ya Kristo Yesu pamoja nami![#Tume. 18:2,18,26.]
4Hao walijitoa wenyewe, wakatwe vichwa, nisiuawe mimi. Mwenye kuwashukuru si mimi peke yangu, ila hata wateule wote walioko kwenye wamizimu.
5Nisalimieni hata wateule waliomo nyumbani mwao! Nisalimieni mpenzi wangu Epeneto! Ndiye aliyeanza kumtegemea Kristo katika Asia.[#1 Kor. 16:15,19.]
6Nisalimieni Maria aliyetusumbukia sana!
7Nisalimieni ndugu zangu Andoroniko na Yunia waliokuwa wamefungwa pamoja nami! Nao ni waelekevu machoni pa mitume, tena walinitangulia kumtegemea Kristo.[#2 Kor. 8:23.]
8Nisalimieni Ampuliato aliye mpenzi wangu katika Bwana!
9Nisalimieni Urbano, mwenzetu wa kazi katika Kristo, na mpenzi wangu Staki!
10Nisalimieni Apele aliyejulikana kuwa Mkristo wa kweli! Nisalimieni wale wa Aristobulo!
11Nisalimieni ndugu yangu Herodio! Nisalimieni wale wa Narkiso wanaomkalia Bwana!
12Nisalimieni Tirifena na Tirifosa wanaosumbuka kwa ajili ya Bwana! Nisalimieni mpendwa Persisi kwa kuwa mwanamke aliyesumbuka sana kwa ajili ya Bwana!
13Nisalimieni Rufo aliyechaguliwa na Bwana, naye mama yake aliye hata mama yangu![#Mar. 15:21.]
14Nisalimieni Asinkrito na Fulego na Herme na Patiroba na Herma na ndugu walio pamoja nao!
15Nisalimieni Filologo na Yulia na Neri na dada yake na Olimpa nao watakatifu wote walio pamoja nao!
16Msalimiane ninyi kwa ninyi na kunoneana, kama watakatifu wanavyozoea! Wateule wote wa Kristo wanawasalimu.[#1 Kor. 16:20.]
17Lakini nawahimiza, ndugu, mwakague wenye matata na makwazo! Hawaushiki ufundisho, mliofundishwa, mwaepuke na kuwaacha![#Mat. 7:15; Tit. 3:10.]
18Kwani watu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, ila huyatumikia matumbo yao wenyewe. Nao kwa maneno yao yaliyo mazuri na matamu mno huidanganya mioyo yao wale wasiojua ujanja.[#Ez. 13:18; Fil. 3:19; Kol. 2:4.]
19Kwani usikivu wenu umejulikana kwa watu wote; hivyo ninawafurahia. Lakini nataka, mwe werevu wa kweli, mambo yenu yawe mema, tena mwe wachanga wasioingia maovu.[#Rom. 1:8; 1 Kor. 14:20.]
20Naye Mungu mwenye utengemano atamponda Satani miguuni penu upesi. Upole wa Bwana wetu Yesu uwakalie ninyi![#Rom. 15:33.]
21Wanaowasalimu ninyi ni Timoteo aliye mwenzangu wa kazi na Lukio na Yasoni na Sosipatiro walio ndugu zangu.[#Tume. 16:1-2; 19:22; 20:4; Fil. 2:19.]
22Mimi Tertio niliyeiandika barua hii nami ninawasalimu ninyi kwa hivyo, ninavyomkalia Bwana.
23Anawasalimu Gayo aliye mwenyeji wangu mimi na mwenyeji wa wateule wote. Naye Erasto aliye mshika mali za mji na ndugu Kwarto wanawasalimu.[#Tume. 19:22; 1 Kor. 1:14.]
24Upole wa Bwana wetu Yesu Kristo uwakalie ninyi nyote! Amin.
25Mungu ndiye anayeweza kuwashikiza ninyi kwa nguvu ya Utume mwema wa Yesu Kristo, ninaoutangaza, kwani nimefumbuliwa mambo ya fumbo yasiyosemwa kale na kale.[#Ef. 1:9; 3:5,9.]
26Yayo hayo yamefumbuliwa sasa na Maandiko ya Wafumbuaji kwa agizo lake Mungu, mwenye kuwapo kale na kale, wamizimu wote wafunzwe huo usikivu wa kumtegemea.[#Rom. 1:5; 2 Tim. 1:10.]
27Yeye Mungu aliye peke yake mwenye werevu wa kweli atukuzwe kwa ajili ya Yesu Kristo kale na kale pasipo mwisho! Amin.[#1 Tim. 1:17; Yuda 25.]