The chat will start when you send the first message.
1Kristo anajua: nasema kweli, sisemi uwongo; hata moyo wangu unaoyajua hunishuhudia katika Roho takatifu,
2ya kuwa masikitiko yangu ni makubwa, nao uchungu haukomi moyoni mwangu.
3Kwa hiyo naliomba mara kwa mara, mimi mwenyewe niapizwe, niondolewe kwake Kristo, kama hivyo vingeweza kuwaponya ndugu zangu, ambao tulizaliwa nao kimtu.[#2 Mose 32:32.]
4Kweli ndio Waisiraeli, tena ni wana, hata utukufu wanao, walipewa maagano na maonyo na tambiko lililo la kweli na viagio.[#2 Mose 4:22; 40:34; 5 Mose 7:6; 14:1; 2 Mose 4:22; 40:34.]
5Wanao hata baba, namo miongoni mwao ndimo, Kristo alimozaliwa kimtu; huyu ni mkubwa kuwapita wote, ni Mungu, atukuzwe kale na kale! Amin.[#Mat. 1; Luk. 3:23-38; Yoh. 1:1.]
6Lakini sisemi hivyo, kwamba Neno lake Mungu limetenguka. Kwani walio kizazi chake Isiraeli sio wote Waisiraeli.[#Rom. 2:28; 4 Mose 23:19.]
7Wala walio wa uzao wake Aburahamu sio wote hata watoto. Ila imeandikwa:
Watakaoitwa uzao wako ni wa Isaka tu.
8Ni kwamba: Walio watoto wa kimtu hao sio watoto wake Mungu; ila walio watoto wa kiagio huwaziwa kuwa uzao.[#Gal. 4:23.]
9Kwani neno la kiagio ni hilo la kwamba:
Nitakapokuja siku zizi hizi za mwaka ujao, ndipo,
Sara atakapokuwa mwenye mtoto wa kiume.
10Lakini hivyo haikuwa hapo tu, ilikuwa napo hapo, Rebeka alipopata mimba kwake yule mmoja aliye baba yetu Isaka.[#1 Mose 25:21.]
11Kwani hapo, watoto walipokuwa hawajazaliwa, wala hawajafanya mema au maovu, hapo ndipo, Mungu alipowachagulia kwa hivyo, alivyowawekea kale, viwepo.
12Vikawapo, si kwa ajili ya matindo yao, ila kwa wito wake yeye. Kwa hivyo Rebeka aliambiwa:
Mkubwa atamtumikia nduguye.
13Ndivyo, ilivyoandikwa:
Nilimpenda Yakobo, lakini Esau nilimchukia.
14Basi, tusemeje? Kwa Mungu uko upotovu? La, sivyo![#5 Mose 32:4.]
15Kwani anamwambia Mose:
Nitakayemhurumia, nitamhurumia kweli; nitakayemwonea
uchungu, nitamwonea uchungu wa kweli.
16Kwa hiyo kutaka kwa mtu siko, wala mbio zake sizo, ila Mungu mwenye huruma ndiye yeye tu.[#Ef. 2:8.]
17Kwani Maandiko yanamsema Farao:
Kwa sababu hiihii nimekuweka, niionyeshe nguvu yangu
kwako wewe, Jina langu lipate kutangazwa katika nchi
zote.
18Kwa hiyo humhurumia, anayemtaka; tena humshupaza, anayemtaka.[#1 Petr. 2:8-9; 2 Mose 4:21.]
19Labda utaniambia: Mbona hutukamia? Kwani yuko nani ayapingaye mapenzi yake?
20Mwenzangu, u mtu gani ukitaka kubishana na Mungu? Je? Kiko chombo kitakachomwambia muumbaji: Mbona umenifanya hivi?[#Yes. 45:9.]
21Mfinyanzi haufanyishi udongo, kama anavyotaka? Donge lililo moja upande mmoja haliumbi kuwa chombo kizuri, nao upande mwingine kuwa kibaya?
22Inakuwaje? Ni kweli, Mungu anataka kuyaonyesha makali yake, tena anataka kuutambulisha uwezo wake, lakini kwa uvumilivu wake mwingi aliwavumilia walio vyombo vitakavyo makali tu, vilivyotengenezwa, viangamie tu.[#Rom. 2:4.]
23Kisha anataka kuutambulisha hata wingi wa utukufu wake kwao walio vyombo vitakavyo huruma, ndio, aliowapatia utukufu kale;[#Rom. 8:29; Ef. 1:3-12.]
24nao ndio, aliowaita kwenye Wayuda nako kwenye wamizimu, nasi tumo.
25Ndivyo, anavyosema hata kinywani mwa Hosea:
Aliitwa: Si ukoo wangu nitamwita: Ukoo wangu,
naye asiyependwa nitamwita Mpendwa.
26Itakuwa hapo, hao wanaoambiwa sasa: Ninyi ham ukoo wangu,
waambiwe: M wanawe Mungu aliye Mwenye uzima.
27Naye Yesaya anawasemea Waisiraeli na kupaza sauti:
Wana wa Waisiraeli ijapo wawe wengi kama mchanga wa
ufukoni,
watakaookoka watakuwa sao tu.
28Kwani Bwana ndiye atakayevimaliza,
atakapolitimiza Neno lake nchini kwa kulikata.
29Navyo ndivyo, Yesaya alivyosema kale:
Bwana Mwenye vikosi kama asingalitusazia uzao,
tungalikuwa kama Sodomu, tungalifanana na Gomora.
30Basi, tusemeje? Ni hivi: Wamizimu wasiofuata wongofu wamepata wongofu; ni wongofu ule unaopatikana kwa kumtegemea Mungu.[#Rom. 10:20.]
31Lakini Waisiraeli walioyafuata Maonyo yenye wongufu hawakuyafikia hayo Maonyo.[#Rom. 10:2-3.]
32Kwa sababu gani? Kwa sababu walikataa kumtegemea Mungu, wakafanya mambo yao tu. Wakajigonga katika lile jiwe la kujigongea,
33kama ilivyoandikwa:
Tazama, naweka humo Sioni jiwe la kujigongea
na mwamba wa kujikwalia.
Naye alitegemeaye hatatwezeka.